LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 16, 2021

MWENYEKITI WA UVCCM KHERI JAMES ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO NYUMBANI KWA MAREHEM MUHAMMED SEIF KHATIB, ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Kheri James akisaini Kitabu Cha Maombolezo nyumbani kwa Marehemu Mohammed Seif Khatibu, Magomeni, katika Wilaya ya Amani mjini Zanzibar, jana.


Unguja, Zanzibar

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Kheri James amesain kitabu Cha Maombolezo nyumbani kwa Marehemu Mohammed Seif Khatibu, Magomeni, katika Wilaya ya Amani mjini Zanzibar.


Marehemu komred Mohammed Seif khatibu  wakati wa uhai wake amehudumu katika Umoja wa Vijana akiwa mwenyekiti wa Kwanza alieongoza kwa kipindi cha mwaka 1978- 1982 na kuhudumu Kwa nafasi ya ukatibu Mkuu wa UVCCM mwaka 1982-1988.


Marehemu Mohammed Seif Khatibu ambaye alifariki jana, atazikwa siku ya leo katika kijiji Cha Umbuji Visiwani Zanzibar .


"Sisi sote ni wa Mungu na kwake tutarejea"

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages