Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amewakabidhi CCM mkoa wa Arusha gari mpya aina ya V8 Land Cruizer, baada ya Mkoa huo kufanya vizuri katika kulinda, kukuza na kubuni miradi ya maendeleo ya Chama, ikiwa ni pamoja na kuongeza vyanzo vya mapato.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo tarehe 10 Februari, 2021 Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.
"Mwenyekiti na Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli ametuhimiza, tuweze kuwekeza nguvu zetu kukifanya Chama kijitegemee kiuchumi, na haya ndio matunda ya maono yake".
Katibu Mkuu amesisitiza kuwa, hii si kwa Arusha peke yake, Dar es salaam wameshanunua gari jipya, mikoa mingine wanaendelea kujenga majengo mazuri, ikiwemo mikoa ya Pwani, Manyara na Geita.
Dkt. Bashiru ametoa rai kwa wanaCCM wote, wakereketwa, Wabunge na Madiwani kuendelea kuwekeza nguvu katika kuimarisha Chama kiweze kujitegemea.
Aidha, Mlezi wa Mkoa huo, ambaye pia ni Katibu Wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndg. Humphrey Polepole, ametumia fursa hiyo kuwashukuru Wakuu wa Chama, kipekee Katibu Mkuu kwa usimamizi mzuri wa utendaji ndani ya Chama ambayo matunda yake sasa yanaonekana.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Ndg. Zelothe Steven amemshukuru katibu Mkuu kwa ushauri na maelekezo ya mara kwa mara katika mkoa wake, na hata kupelekea mafanikio makubwa yanayoanza kupatikana sasa mkoani humo.
Huu ni utaratibu wa kuendelea kukijenga Chama kiuchumi, kiweze kutoa uongozi, ikiwa ni pamoja na kuisimamia serikali kutoa huduma kwa wananchi.
Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).
iMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇