LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 5, 2021

MKURUGENZI MKUU SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR(ZBC) CHANDE OMAR ATUMBULIWA, LEO

CCM Blog, Zanzibar

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita kwa maelekezo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametengeua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Chande Omar 


Utenguzi huo unakuja kufuatia ripoti ya kamati ya Uchunguzi iliyoundwa tarehe 17 Disemba 2020 kwa ajili ya kuchunguza mambo mbalimbali yaliyopo katika Shirika hilo


Tabia amesema Kamati hiyo imebaini mambo mbalimbali ambayo ni ukiukwaji wa sheria na taratibu za nchi ikiwemo kuajiri wafanyakazi wasio na sifa katika shirika hilo


Aidha Kwa mujubu wa maelekezo ya Rais wa Zanzibar amevunja Bodi ya Shirika la Utangazaji ZBC na kumteua Ali Uki kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages