LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 8, 2021

MJUMBE MPYA WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU LIBYA AANZA KAZI RASMI

 

  • Mjumbe mpya wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya aanza kazi rasmi Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya leo Jumatatu, Februari 8, 2021 ameanza kazi rasmi.

Ján Kubiš ndiye mjumbe mpya maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, AntĂłnio Guterres katika masuala ya Libya na leo leo amefanya mazungumzo na Fayez al Sarraj, Rais wa Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa na akatilia mkazo wajibu wa kuundwa haraka Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo itasimamia Uchaguzi Mkuu wa tarehe 24 Disemba mwaka huu. Katika mazungumzo yao, wawili hao wamesisitizia pia umuhimu wa kuweko mazungumo pia ya kijeshi na kiusalama baada ya kuundwa serikali hiyo mpya na kuitishwa uchaguzi mkuu katika tarehe iliyopangwa, bila ya kuakhirishwa hata siku moja.

Wababe wawili wakuu wa kivita nchini Libya

Sarraj na Kubiš wamebadilishana mawazo pia kuhusu matukio ya hivi karibuni ya Libya na kuelezea matumaini yao kwamba, baada ya kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, taasisi nyingine zote muhimu za kiutawala za Libya, nazo zitaweza kuunganishwa chini ya serikali hiyo. Kabla ya kuanza rasmi kazi zake, Ján Kubiš amefanya mazungumzo pia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya, Mohamed Taher Siala. Ghassan SalamĂ©, mjumbe wa zamani wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya alijiuzulu wadhifa wake mwezi Machi 2020 baada ya kushindwa juhudi zake za kukomesha mapigano nchini humo. Libya hivi sasa ina serikali mbili. Moja ni ile yenye makao yake huko Tripoli mji mkuu wa nchi hiyo chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Fayez al Sarraj. Serikali hiyo inatambuliwa rasmi na kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa na nyingine ina makao yake katika mjini Tobruk mashariki mwa nchi hiyo ikiungwa mkono na Imarati, Misri, Saudi Arabia na nchi kadhaa za Ulaya. 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages