LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 14, 2021

MAMA SAMIA AWAHAKIKISHIA NEEMA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WAKUBWA.

 

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akimsikiliza kwa makini, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe aliyekuwa akimweleza jambo, wakati wa ziara yake katika Wilaya hiyo, leo.


Temeke, Dar es Salaam

Serikali imewahakikishia mazingira mazuri ya kufanyia biashara, wafanyabiashara  wadogo na wakubwa nchini huku akisisitiza kuondolewa kwa kodi na ushuru ambao ni kero kwa wafanyabiashara hao.


Neema hiyo kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa imesemwa na Makamu wa Rais Samia Sulu Hassan akiwa katika ziara ya kikazi, kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa masoko katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.


Samia Suluhu alisema, Serikali katika kutekeleza kwa vitendo Ilani ya CCM  iliamua kuanzisha utaratibu wa vitambulisho vya wajasiriamali ambavyo vinawawezesha kulipa kwa awamu moja tu kwa mwaka na kusaidia kupunguza mzigo kwa wafanyabiashara hao.


"Lakini kama mlivyosikia Waziri Mkuu, alikuwa na mkutano na wawakilishi wa wajasiriamali wa Tanzania nzima ili kuangalia nini Serikali yenu inaweza kufanya kuboresha mazingira ya kufanya biashara".Aliongeza Mama Samia Suluhu Hassan.


Katika hatua nyingine Makamu wa Rais aliupongeza uongozi wa manispaa hiyo kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato lakini akiwakumbusha kuwa fedha hizo ziende kutatua kero na changamoto za wananchi.


Awali akimkaribisha Makamu wa Rais, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Aboubakar Kunenge alieleza kuwa Manispaa ya Temeke imepiga hatua kimaendeleo ikilinganisha na miaka iliyopita.


"Katika serikali hii ya awamu ya tano tunaona wilaya hii imepata maendeleo sana na inakuwa kwa kasi kubwa, kwa kweli nampongeza sana Rais." Alisema Mh.Kunenge


Katika ziara hiyo ambayo  Makamu wa Rais alianzia katika wilaya ya Kigamboni, aliweza kukagua miradi ya barabara Kijichi, kituo cha kibiashara na soko Kijichi pamoja na masoko mengine ya Makangarawe, Mbagala kuu, pamoja na soko la Kilakala yote yakiwa katika Manispaa  ya Temeke.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages