Makumi ya watu wametoweka na kuhofiwa kufariki baada ya donge kubwa la barafu kuvunja bwawa na kusababisha mafuriko makubwa katika eneo la kaskazini mwa India.
Bwawa hilo lililovunjika lilisababisha mafuriko makubwa kumwagika katika bonde moja katika jimbo la Uttarakhand.
Wanavijiji wameondolewa , lakini maafisa wameonya kwamba huenda zaidi ya watu 150 wameathiriwa na mafuriko hayo.
Kanda za video zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zilionesha mafuriko hayo yakipita katika eneo hilo na kufanya uharibifu mkubwa.
"Yalikuja haraka , hakukuwa na muda wa kuwatahadharisha watu'' , Sinjay Singh Rana ambaye anaishi katika kijiji cha karibu aliambia chombo cha habari cha Reuters.
Waziri mkuu Narendra Modi amesema kwamba anachunguza hali . ''Taifa liwaombee kila mtu aliyeko katika eneo hilo'' , alindika katika mtandao wake wa Twitter, muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na mawaziri wa jimbo hilo.
Wafanyakazi wa dharura wanawaondoa makumi ya wanavijiji huku wakiendelea kuingia katika handaki moja lililozibwa ili kuwaokoa watu waliokuwa wamezuiwa ndani yake.
''Kiwango cha maji ya mto huo sasa ni mita moja juu ya kiwango cha kawaida lakini mtiririko wake unapungua'', waziri mkuu wa Uttarakhand Trivendra Signh Rawat alisema baadaye siku ya Jumapili.
Wakati huohuo, Jimbo jirani la Uttar Pradesh pia lilitoa notisi ya hali ya tahadhari kwa wakaazi wake wanaoishi kandokando ya mito.
Jimbo la Uttarakhand lililopo , magharibi mwa Himalayas ni eneo linalokumbwa na mafuriko pamoja na maporomoka mara kwa mara.
Takriban watu 6000 wanaaminika kuuawa katika mafuriko mwezi Juni 2013 ambayo yalisababishwa na mvua za vuli katika miongo kadhaa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇