LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 17, 2021

DK SERAPHIA AMUELEZEA RAIS DK MWINYI, MKURABITA ITAKAVYOWAKOMBOA WANYONGE KIUCHUMI ZANZIBAR


MRATIBU wa Mpango wa Kurasimisha Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), Dk Seraphia Mgembe (kulia) akimuelezea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi kuhusu nia na mikakati ya Mkurabita kusaidia kuwakomboa wanyonge kiuchumi katika visiwa vya Unguja na Pemba kwa kurasimisha ardhi na biashara zao pamoja na kuwapatia mafunzo ya jinsi ya kuendesha biashara zao.
Dk. Seraphia alipata fursa hiyo ya kueleza mbele ya Rais Mwinyi baada ya Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Kamati ya Uongozi ya mpango huo, Immaculata Senje (kulia kwake) kusoma taarifa ya Mkurabita ya utekelezaji wa urasimishaji wa mali za wanyonge Zanzibar na Tanzania Bara wakati Wajumbe wa Bodi hiyo, kukutana na Rais huyo Ikulu Zanzibar Februari 11,2021. Mdau ili nisikuondolee uhondo nakuomba uendelee kumsikiliza Dk. Seraphia akielezea mbele ya Rais Mwinyi kuhusu nia na mikakati hiyo kupitia clip hii ya video.... Imeandaliwa na Richard Mwaikenda Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 0754264203



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages