Mabingwa wa kihistoria Ligi Kuu Tanzania bara wamezidi kujiimarisha baada ya kunasa saini ya beki chipukizi wa Klabu ya Mtibwa Sugar Dickson Job ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili .
Chini ya Kocha Mkuu Cedrick Kaze ambaye ameendelea kukiboresha kikosi hicho ambacho kinaongoza msimamo wa Ligi Kuu huku kikiwa hakijapoteza hata mechi mmoja.
Job anaungana na rafiki yake Kibwana Shomari ambaye walicheza kwa pamoja katika timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 Serengeti boys kilichoshiriki michuano ya AFCON 2017 nchini Gabon ambaye naye alijiunga na Yanga mwaka jana.
Job kwa sasa yupo kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya DR Cong, kesho katika uwanja wa Mkapa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇