LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 21, 2021

WIZARA, BODI WAMPONGEZA KAIMU MKURUGENZI DUWASA, ARON KWA UCHAPAKAZI BORA

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi akipongezana na Kaimu Mkurugenzi wa Duwasa, Aron Joseph  baada ya kuzindua Baraza la 6 la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo Januari 20,2021 jijini Dodoma. Katika hotuba yake, Mhandisi Mahundi alimpongeza Aron kwa utendaji wake mzuri.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mwenyekiti wa Bodi ya Duwasa, Prof. Faustine Bee akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza hilo ambapo pia alimpongeza Aron Joseph kwa uchapakazi wake tangu ateuliwe kuongoza mamlaka hiyo.

 Naibu Waziri Mhandisi Mahundi akijadiliana jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Duwasa, Aron
.



Na Richard Mwaikenda, Dodoma

NAIBU Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi amempongeza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa  Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA),, Aron Joseph kwa uchapakazi.

 

Naibu Waziri Mahundi ametoa pongezi hizo  wakati wa uzinduzi wa Baraza la 6 la Wafanyakazi wa Duwasa kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), jijini Dodoma  Januari 20, 2021.

 

Akitoa pongezi hizo, Naibu Waziri Mhandisi Mahundi amesema tangu yeye ameingia madarakani, kila akiwasiliana naye amekuwa na mwitikio mzuri kitendo ambacho kinaonesha utendaji wake ni mzuri.

 

Pongezi zingine kwa  Aron Joseph zimetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka hiyo,  Profesa Faustine Bee ambaye alisema tangu Kaimu Mkurugenzi huyo ateuliwe kwa nafasi hiyo amekuwa akionesha ushirikiano mkubwa katika utendaji kazi.

 

“Mheshimiwa Naibu Waziri tunashukuru uongozi wa wizara kwa kutuletea mchapakazi bora Aron, karibu sana Aron. Sisi kwenye Bodi tutaendelea kukupa ushirikiano  lakini pia  mameneja na timu nzima ya menejimenti pamoja na wafanyakazi watafanya hivyo katika kufikia azma kwa kuifanya mamlaka kuwa  bora, yenye kutoa huduma bora iliyotukuka…

 

Niwaombe wajumbe na wafanyakazi tumpe  ushirikiano wa kutosha ili aweze kutekeleza majukumu aliyopewa,”Prof. Bee alimpongeza Aron.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages