Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza katika kikao kazi na menejimenti ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) jijini Dodoma leo Januari 15, 2021. Kikao hicho kimehudhuriwa na mameneja wa TTCL kutoka mikoa yote nchini. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa wizara hiyo, Prisca Olomi akiratibu kikao hicho.
Wajumbe wa kikao hicho wakiomba dua kabla ya kuanza kikao kwa lengo la kukipa baraka.
Sehemu ya mameneja wa mikoa wakiwa katika kikao hicho.
Waziri Ndugulile akitoka baada ya kufungua kikao hicho cha menejimenti.
Dkt. Ndugulile akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa TTCL, Waziri Kindamba.
WAZIRI wa
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile ametangaza wazi
kuingia mkataba na wenyeviti wa bodi na wakurugenzi watendaji wa Taasisi
zilizopo chini ya wizara hiyo ili kupima uwajibikaji wao.
Dkt.
Ndugulile ametangaza mkataba huo wakati wa kikao kazi cha menejimenti ya Shirika
la Mawasiliano Tanzania (TTCL), yenye mameneja wa chi nzima, kilichofanyika
jijini Dodoma Januari 15, 2021.
Amesema mkataba huo utakuwa kupimana utendaji kila baada ya miezi mitatu lengo likiwa kuongeza uwajibikaji katika Taasisi hizo na
kuleta matokeo yanayopimika.
Waziri
Dkt.Ndugulile ambaye katika kikao hicho aliambatana na Naibu Katibu Mkuu wa
wizara, Dk. Jim Yonazi pamoja na baadhi ya maofisa wa wizara hiyo, amesema ndani
ya siku hizo tisini wamueleze wamefanya
nini kinachopimika cha kwenda kuwaambia wananchi.
Amewataka
wakurugenzi nao wabanane kwa kuwapa malengo mameneja wao kuhakikisha
wanaongeza wigo kwa wateja na kuboresha
huduma pamoja na kuzisapoti bidhaa walizozianzisha.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TTCL, Waziri Kindamba, alisema moja ya kazi nzuri
iliyofanywa na menejimenti kwa miaka
michache iliyopita ni mabadiliko ya kuitoa taasisi katika kuingiza hasara na
kuifanya iingize faida.
Amesema kuwa
timu hiyo ya menejimenti imekuwa kinara wa kuongeza mafanikio yanayotokea katika shirika hilo
kutoka kupata hasara sh. Bilioni 15 kila mwezi na sasa
kupata faida ya sh. Bilioni 5 kila mwezi.
Dkt.
Ndugulile amesema jambo lingine ambalo menejimenti imefanya katika mabadiliko
ya TTCL ni kuongeza mapato kutoka Sh. Bilioni 85 hadi kufikia
sh. Bil. 149 kwa sasa.
Lakini pia,
Kindamba ameelezea jinsi TTCL ilivyofanikisha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020
kwa matokeo kutoka ndani ya masaa 48 na kuhakikisha mchakato hauingiliwi na
mataifa ya nje.
Ndugu ndugu nakuomba uendelee kumsikiliza Dkt Ndugulile kwenye clip hii ya video....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇