LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 26, 2021

WAUMINI WA KANISA LA BAPTIST KAGERA WAMLILIA RAIS MAGUFULI MGOGORO WA ARDHI ULIODUMU KWA MIAKA 20 MALI YA KANISA ILIMOJENGWA SHULE YA MSINGI .

Waumini wa Kanisa la BAPTIST Omurushaka wilayani Karagwe Mkoani Kagera aliyenyoosha mkono ni mchungaji wa Kanisa hilo na meneja wa shule ya msingi bohari Mchungaji Dionizi Karwani
  Na Mwandishi wetu 

Waumini wa Kanisa la Baptist Omurushaka wilayani  Karagwe Mkoani Kagera wamemuomba Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli kuunda tume ya kuchunguza mgogoro wa ardhi wa kiwanja ,Mali ya Kanisa hilo eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya shule ya msingi bohari baada ya Kanisa hilo kushinda kesi kadhaa bila kupata muafa tangu mwaka 2003.


Wakizungumzia Hali hiyo waumini wa Kanisa hilo akiwemo Nelson Wilson, Pius Beichumila Clementina Deus na Speratu Tshema wamesema mgogoro ulioanza mwaka 2003 ni Kati ya mshitaki / mdai ambaye Ally Chamani mwanasheria wa mahakama kuu ya Bukoba Mkoani Kagera na Kanisa la Baptist mgogoro ambao wamedai kuwa licha ya kushinda kesi kadhaa hauonyeshi mafanikio umeathili huduma ya Kanisa pamoja na shule kwani wanafunzi upata Elimu kwa wasi wasi hivyo kumuomba Rais Magufuli kuingilia Kati ili huduma ya jamii iendelee.


Akizungumzia Hali hiyo mchungaji wa Kanisa la Baptist Omurushaka Karagwe Dioniz Karwani amesema kuwa katika kesi hiyo no 3 ya mwaka 2003 alimshtaki mkurugenzi wa wilaya ya Karagwe Godwin Kitonka pamoja na Kanisa hilo ambapo aliipeleka mahakama ya wilaya ya Karagwe na baadaye muhusika kushindwa .


Amesema kuwa 2003 muhusika alikata rufaa katika mahakama kuu ya Bukoba kesi no 15 ya mwaka 2006 chini ya Jaji PB   Khaday ambapo mdai alishindwa.


Karwani ameongeza kuwa baada ya mshitaki kushindwa aliamua kufungua kesi hiyo kwa Mara nyingine katika mahakama kuu ya Bukoba kesi no 29 ya mwaka 2014 chini ya Jaji SB Bongole J na kushindwa Kisha kudai kulipa madai ambayo aliikatia rufaa kukataa gharama za kesi hiyo nayo akashindwa, na kuamua kufungua kesi katika mahakama kuu ya Bukoba yenye namba 6 ya mwaka 2018 chini ya Jaji N.N Kilekamajenga  na pia kushindwa.


Mchungaji Karwani  amesema kuwa mdai huyo ambaye ni mwanasheria aliamua kufungua tena kesi no 60 ya mwaka 2016 na kushindwa na kuwa 2021 amefungua kesi no 3 na kesi no 67 ya mwaka 2020 ambazo ziko mahakama kuu ya Bukoba.


Mchungaji wa Kanisa hilo na meneja wa shule ya msingi bohari iliyojengwa katika kiwanja hicho chenye mgogoro amesema kwa anachokiomba  kwa Rais Magufuli ni kuchunguza mgogoro kwa kuundwa tume itakayosaidia mgogoro huo kuisha .


" Vibali vyote vipo  Kanisa  limelipia hata stakabadhi za kiwanja hicho miaka yote na kiwanja kilinunuliwa na kimeisha pata ofa hapa uwenda Kuna rushwa na uzembe Rais wetu ni msikivu mpenda maendeleo atatusaidia" alisema mchungaji Karwani


Aidha ameongeza kuwa Kanisa kwa kuwa lilitaka maendeleo lilifanya mabadiliko kwa wziri mkuu wa Tanzania Kassimu majaliwa mwaka 2005 kuwa matumizi ya kiwanja kwa matumiza ya shule ambapo pia tume kutoka halmashauri ya wilaya ya Karagwe iliundwa ili kufuatikia kiwanja hicho na kulidhia kuwa kiwanja hicho ni Mali ya Kanisa ambapo wahusika waliandaliwa barua juu ya kujenga isivyo halali katika kiwanja No  100 kitalu D.


Hata hivyo kwa upande wake mshitaki Ally Chamani (mwanasheria)akiongea na blog ya taifa kwa njia ya simu amesema kuwa kesi hiyo inaendelea mahakamani ambapo amedai kuwa mwanzoni alifungua kesi hiyo lakini alishtaki kisheria mtu ambaye hayupo duniani .

1 comment:

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages