Watu 5 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 3 kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa kilipuzi kilichokuwa kimetegwa barabarani katika mkoa wa Tebse, eneo la mpakani mwa Algeria na Tunisia.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Algeria, iliarifiwa kwamba kilipuzi hicho kilichotegwa kando ya barabara mkoani Tebse, kililipuka wakati gari la raia lilipokuwa likipita.
Taarifa zaidi zimefahamisha kwamba watu 5 walifariki na wengine 3 walijeruhiwa kwenye mlipuko huo.
Baada ya shambulizi hilo, vikosi vya jeshi vilipelekwa katika eneo tukio na uchunguzi ukaanzishwa.
Maeneo ya mpakani mwa Algeria na Tunisia yamekuwa yakikumbwa na mashambulizi yanayoendeshwa na vikundi vilivyofungamana na shirika la kigaidi la Al Qaeda kwa miaka mingi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇