Meneja kitengo cha Biashara ya Kadi Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa akizungumza kwenye droo ya MastaBata leo katika ofisi za Benki ya NMB Makao Makuu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Pendo Mfuru akisimamia droo hiyo na kulia ni Afisa Huduma kwa Wateja, Yvette Nkhoma.
Afisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Yvette Nkhoma (kulia) akibofya kitufe kumpigia simu mmoja wa washindi wa droo ya Mastabata si Kikawaida, alioibuka mshindi katika droo ya wiki ya sita iliyoendeshwa leo. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Pendo Mfuru akisimamia droo hiyo na katikati ni Meneja kitengo cha Biashara ya Kadi Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa.
Afisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Yvette Nkhoma (kulia) akizungumza na mmoja wa washindi wa droo ya Mastabata si Kikawaida, alioibuka mshindi katika droo ya wiki ya sita iliyoendeshwa leo. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Pendo Mfuru akisimamia droo hiyo na katikati ni Meneja kitengo cha Biashara ya KadiBenki ya NMB, Sophia Mwamwitwa.
*********************************************
NA MWANDISHI WETU
DROO ya sita ya Kampeni ya NMB MastaBATA, inayoendeshwa na Benki ya NMB, imefanyika jijini Dar es Salaam, ambako washindi 40 wamepatikana na kufanya idadi yao tangu kuanza kwake Novemba 2020, kufikia 240.
NMB MastaBATA, ni Kampeni ya miezi mitatu iliyozinduliwa Novemba 24, 2020 na itadumu hadi Februari mwaka huu, ambako zawadi mbalimbali zinatolewa zikiwamo pesa, simu janja, jokofu, runinga na safari ya kwenda kupumzika Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro.
Droo hiyo imesimamiwa na Pendo Albert, kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), ambako washindi wamejinyakulia Sh. 100,000 kila mmoja, kigezo cha ushiriki kikiwa ni matumizi ya Kadi za NMB Mastercard na Mastercard QR.
Akizungumza kabla ya kufanyika kwa droo hiyo, Meneja wa Idara ya Kadi ya NMB, Sophia Mwamwitwa, alisema jumla ya washindi 200 walishapatikana katika droo tano za kila wiki, na kwamba kampeni nzima inalenga kuzawadia washindi 400.
Aliongeza kuwa, ukiondoa droo za kila wiki, pia NMB MastaBATA imewazawadia jumla ya washindi 12 kati ya washindi 15 wa droo za kila mwezi ambao wao wamekuwa wakijishindia simu janja aina ya Samsung Galaxy Note20, yenye thamani ya Shilingi Mil. 2.4
“Wito wetu kwa wateja wa NMB wenye kadi za NMB Mastercard na Masterpass QR, kufanya manunuzi na malipo mbalimbali ili kujiwekea nafasi ya kushinda droo zijazo za kila wiki, kila mwezi na ile zawadi kuu ya Grand Finale,” alisema Mwamwitwa.
Aidha, zawadi kuu ya Grand Finale ambayo ni utalii Zanzibar, Ngorongoro ama Serengeti, inawapa washindi uhuru wa kuchagua zawadi mbadala kama runinga iliyolipiwa DSTV miezi mitatu, Jokofu, Laptop, Simu (Samsung A70), Water Dispenser na Microwave.
Kwa upande wake, Pendo, Ofisa wa GBT, aliwataka wateja wa NMB kuendelea kutumia kadi zao ili kujishindia zawadi zinazotolewa na NMB MastaBATA, na kwamba mchakato wa kuwapata washindi unafanyika kwa kufuata sheria na taratibu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇