LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 17, 2021

UPANDAJI MITI DODOMA SI JAMBO LA HIARI NI LAZIMA-RC MAHENGE+video

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge (kulia) akisaidiana na Meneja wa Wakala wa Misitu (TFS) Kanda ya Kati, Mathew Kiondo kupanda mti katika eneo la wazi la Iseni Park, jijini Dodoma Januari 16,2021. Jumla ya miti 3700 iiyotolewa na TFS imepandwa katika eneo hilo lenye ukuwa wa heka 37. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Wananchi na viongozi mbalimbali wakishiriki upandaji miti eneo la Iseni Park jijini Dodoma.
RC Mahenge akitoa shukrani kwa watu wote waliojitokeza kupanda miti katika eneo hilo Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Josephat Maganga.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Chuo Kikuu cha Dodoma, Kitivo cha Elimu, Godfrey Masele akipanda mti.












Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Mipango Dodoma wakipanda mti


Mmoja wa wapenzi wa Klabu ya Yanga, akiwa na miti tayari kushiriki kuipanda


Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru akielezea historia ya eneo la wazi la Iseni Park na jinsi litakavyoboreshwa kwa kupanda miti na kuitunza ili kuifanya bustani hiyo kuwa ya kuvutia.

 Mratibu wa Wakala wa Barabara Vijijini, Mhandisi Lusako Kilembe akielezea jinsi watakavyopanda miti kwenye barabara wanazozijenga jijini Dodoma. Katikati ni Mjume wa Halmashauri Kuu ya Taifa  ya  CCM, Ahidi Sinene.


Na Richard Mwaikenda, Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge amesema kuwa kazi ya upandaji miti katika mkoa huo si  jambo la hiari bali la lazima kwa kila mtu.

Ameagiza viongozi wa kila kata katika mkoa huo kusimamia kazi ya upandaji miti kila Jumamosi hasa wakati huu wa msimu wa mvua, isipokuwa Jumamosi ya mwisho wa mwezi ambayo ni siku iliyotengwa maalumu kwa ajili ya usafi.

Ametoa maagizo hayo wakati wa kazi ya upandaji miti eneo la wazi la Iseni Park lililopo nyuma ya jengo la Hazina jijini Dodoma Januari 16,2021. Jumla ya miche 3700 iliyotolewa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), imepandwa.

Dkt Mahenge amesema ni wajibu kwa kila mtanzania kuona umuhimu wa kupanda miti katika maeneo yao kwani ndio ulithi pekee tulioachiwa katika sayari hii.

“Tangu sayari hii iumbwe haiongezeki wala kupungua ndio tunayoishi na rasilimali tulizo achiwa na zinazidi kupungua, mito mingi inakauka ni wajibu wetu kuendelea kulinda” amesisitiza Dkt. Mahenge.

Amesema katika kuendelea kwa Teknolojia hapa Duniani zimeathiri uoto wa asili, ili kurudisha uasilia wa uoto wa asili ni lazima kutunza mazingira na kuendelea kupanda miti katika maeneo yaliyo wazi.

Amewataka watanzania kuendelea kuhamasika katika kulinda mazingira na kujenga utamaduni wa kupanda miti katika maeneo yote hasa katika maeneo ya Mkoa wa Dodoma.


Wakati huo huo, Meneja wa TFS, Kanda ya Kati, Mathew Kiondo amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Mahenge aje azindue kampeni ya umwagiliaji wa miti iliyopandwa hasa wakati wakiangazi ili istawi vizuri.

Kiondo ameomba ushirikiano na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), kuweka matanki ya maji eneo hilo kwa ajili ya umwagiliaji kwenye miti hiyo.



Imeandaliwa na; 
Richard Mwaikenda 
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages