MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dodoma, Ahadi Sinene amesema kupanda miti ni chakula ambacho matunda yake utakula wewe, mdogo wako, mjomba wako na hata shangazi yako.
Sinene aliendesha elimu ya umuhimu wa kupanda miti na faida zake wakati wa kampeni yake ya kupanda miti 250 ikiwemo ya matunda eneo la Mtumba jijini Dodoma. Ilishirikisha wanafunzi na wakazi wa eneo hilo.
Alisema licha ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani lakini pia miti ina faida kwa maisha ya binadamu kwani huzaa matunda ambayo ni chakula, lakini pia huleta vivuli, kupunguza joto na kusababisha mvua, hivyo jambo la kupanda litoke ndani ya moyo wako na liwe endelevu.
Pia alikemea tabia za baadhi ya watu kuharibu mazingira kwa kukata ovyo miti iliyopandwa na kusema kusiwepo na simile ya kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Mdau nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video upate zaidi yaliyojiri kwenye kampeni hiyo ya upandaji miti iliyoongozwa na Sinene....
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇