Baadhi ya mameneja wa TTCL mikoa mbalimbali wakiwa katika kikao hicho wakimsikiliza kwa makini Waziri Ndugulile alipokuwa akikifunga.
Na Richard
Mwaikenda, Dodoma
SHIRIKA la
Mawasiliano Tanzania (TTCL), limejitia kitanzi cha uboreshaji wa shirika hilo kwa
kutangaza maazimio matano mbele ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari, Dk. Faustine Ndugulile watakayoyatekeleza ndani ya mwaka mmoja.
Maazimio
hayo yametangazwa mbele ya waziri jijini Dodoma Januari 17, 2021, na Mkurugenzi
Mtendaji wa shirika hilo, Waziri Kindamba wakati wa kufunga kikao kazi cha siku
tatu cha menejimenti kilichohudhuriwa na mameneja wa TTCL nchi nzima.
Kindamba ametaja
maazimio hayo kuwa ni;Utekelezaji wa Ilani ya chama tawala cha CCM, kuongeza wateja kutoka asilimia mbili ya sasa hadi
asilimia 6 na zaidi ndani ya mwaka mmoja,
watapanua
wigo wa mawakala wa vocha na T Pesa kutoka 2800 hadi 3080 ndani ya miezi
mitatu, lakini vilevile wataboresha kitengo cha huduma kwa wateja hadi ifikapo
Machi mwaka huu.
Maazimio
mengine aliyoyataja ni; uboreshaji wa Kitengo cha Biashara na Matangazo pamoja
na kuimarisha uhusiano na taasisi binafsi za serikali kwa ujumla.
Waziri Dk.
Ndugulile aliyapokea maazimio hayo kwa moyo mmoja na faraja na kuwaeleza kwamba kwa vile
wameazimia wenyewe kufanya hivyo hana shaka kwamba yatatekelezwa kwa ufasaha
ndani ya muda uliopangwa.
Amesema
atafanya ziara nchi nzima kupima matokeo ya utekelezaji wa maazimio hayo na
endapo yatakwenda kinyume, basi yupo tayari kumshughulikia Mkurugenzi Mtendaji
ili nay eye kabla ya kuwajibishwa awashughulikie watendaji walio chini yake.
“Niliwaeleza
kwamba mimi nitaingia mkataba wa uwajibikaji na wakurugenzi watendaji,
usipotimiza malengo mliyojiwekea nitakushughulikia, sasa na wewe kaingie
mikataba na mameneja wako ili kabla ya kushughulikiwa uwashughulikie wao,”amesisitiza
Dk. Ndugulile.
Lakini
vilevile ili uboreshaji huo uende kwa ufanisi Dk. Ndugulile ameahidi kuzitafutia
ufumbuzi baadhi changamoto alizoambiwa ikiwemo uhaba wa magari na vitendea kazi
vingine muhimu.
Ameitaka
TTCL kuandaa mpango mkakati wenye mambo muhimu na bajeti yake na kueleza fedha watakazopewa watazifanyia nini, zitaleta tija gani na kwa
muda gani.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇