Waziri Ndugulile akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi akitoa neno la shukrani wakati wa kuhitimisha kikao hicho kilichofanyika Kituo cha Mikutano cha Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA, akielezea mafanikio ya kikao kazi hicho na jinsi walivyojipanga kutekeleza maagizo ya waziri pamoja na utekelezaji wa ilani ya chama tawala kuhusu kuinua na kuboresha sekta ya mawasiliano nchini.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
SERIKALI
imeazimia kujenga kiwanda cha kutengeneza simu janja mkoani Mwanza ili
kurahisisha mawasiliano nchini kwa
gharama nafuu.
Mpango huo
umetangazwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile
alipokuwa akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kuhusu yaliyojiri kwenye kikao kazi na viongozi wa taasisi sita zilizochini ya
wizara hiyo, jijini Dodoma leo Januari 14, 2021.
“Sisi katika
wizara mpya hatuwezi kusubiri kutumwa
kazi, tumesoma ilani ya chama imesema tuongeze wigo wa mawasiliano ,
tuongeze matumizi ya intaneti , hatuwezi kufanikiwa ikiwa wananchi watashindwa
kununua simu janja na kompyuta mpakato,
na hili tumeliona na serikali hivi sasa imeanza mchakato wa kuanzisha kiwanda
cha kutengeneza simu janja mkoani Mwanza ili wananchi wapate simu kwa gharama
nafuu,” amesema Dkt Ndugulile..
Ametoa rai
kwa wafanyabiashara wenye nia ya kutaka kuwekeza katika sekta ya mawasiliano
waende Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari watapewa ushirikiano wa asilimia
100 kuhakikisha zinatengenezwa bidhaa za Tehama ambazo zinaweza kutumika ndani
ya nchi ili wananchi wengi wazipate kwa gharama nafuu.
Amesema kuwa malengo ni asilimia 70
ya huduma zinazotolewa na Serikali ziwe zinatumia Tehama kupunguza urasimu
ambapo mwananchi badala ya kufuata huduma katika ofisi za serikali, atumie Tehama kulipia kodi kwa kutumia simu janja, mwanafunzi angalie matokeo yake kwenye
mtandao, mkulima aulizie au kununua mbegu kwenye mtandao.
Katika mkutano huo na wanahabari, Waziri amezungumza
mengi kuhusu umuhimu wa matumizi Tehama katika karne hii, hivyo nakusihi endelea kumsikiliza Dkt. Ndugulile kupitia kwenye clip hii ya video….
IMEANDALIWA NA;
Ni hatua njema sana na ya kupigiwa upatu. Tunakwenda kupata mawasiliano bora na uhakika. Suala la gharama za INTERNET bado linaumiza mno.
ReplyDelete