LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 5, 2021

SAHIHISHO: DAWASA YATANGAZA MAENEO MENGI YA DAR NA BAGAMOYO KUKOSA MAJI LEO NA KESHO

 


05/01/2021

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inawataarifu wananchi wa Jiji la Dar es salaam wanaohudumiwa na Mtambo wa uzalishaji Maji wa Ruvu Chini kuwa  kutakuwa na upungufu wa huduma ya Maji kuanzia siku ya Jumanne tarehe 05/01/2021 hadi siku ya Jumatano tarehe 06/01/2021.


Sababu: Kuruhusu usafishaji wa clarifier kazi itakayopelekea upungufu wa uzalishaji maji kwa asilimia 25 na kuathiri huduma ya maji kwa saa 24 katika maeneo yanayo hudumiwa na mtambo huo


Maeneo yatakayoathirika ni: Mji wa Bagamoyo, Vijiji vya Zinga, Kerege, Mapinga, Bunju, Boko, Kawe, Kinondoni, Ilala, Temeke, Uwanja wa Ndege, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach, Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Kijitonyama, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Rufaa Muhimbili na Kigamboni Navy na Ferry.


DAWASA inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


Wasiliana nasi huduma kwa wateja 0800110064 (Bure), 0735 212020 (Whatsap tu)


Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano na jamii- DAWASA

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages