Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi akizindua rasmi Baraza la Sita la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (Duwasa) jijini Dodoma leo Januari 20, 21. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Duwasa, Aron Joseph na Mwenyekiti wa Bodi ya Duwasa, Profesa Faustine Bee. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Kaimu Mkurugenzi wa Duwasa, Aron Joseph akizungumza kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ambaye alimkaribisha mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Duwasa,Prof. Faustine Bee akiungumza na kutaja maazimio ya baraza hilo ya kuiboresha Duwasa.
Naiu Waziri wa Maji, Mhandisi Mahundi akihutubia wakati wa kuzindua Baraza a Wafanyakazi wa Duwasa.
Mhandisi Mahundi akijadiliana jambo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Duwasa, Aron Joseph
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Duwasa wakisikiliza kwa makini wakati Naibu waziri akihutubia.
Naibu Waziri, Mhandisi Mahundi akiwa na wajumbe wa Baraza na viongozi wa Duwasa.
Mahundi akiagana na wajumbe baada ya kupiga nao picha ya pamoja.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
NAIBU Waziri
wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi ameitaka Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na
Usafi wa Mazingira Mji wa Dodoma (DUWASA), isije ikajisahau kwa kufanya kazi za
menejimenti badala ya kuisimamia.
Naibu Waziri
Mahundi ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Baraza la 6 la Wafanyakazi wa
Duwasa kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), jijini Dodoma leo
Januari 20, 2021.
Aidha, Mhandisi
Mahundi amelitaka Baraza la Wafanyakazi la Duwasa kuendelea kuikumbusha Bodi
kuhusu majukumu yake hayo kwa lengo la kuiendeleza mamlaka hiyo.
“Ni wajibu
wa Taasisi za serikali kuwa na mabaraza
ya wafanyakazi kwani yameanzishwa kisheria kuishauri serikali katika ngazi ya idara,
taasisi na ngazi ya wizara kuhusu usimamizi wa kazi na rasilimali watu,”
amesema Naibu Waziri Mahundi.
Alitaja majukumu
mengine ya Baraza kuwa ni,utekelezaji wa
majukumu, kulinda haki na wajibu kwa waajiri na wafanyakazi, kutoa ushauri
kujenga hali bora ya kazi, maslahi bora ya wafanyakazi na kusimamia haki na
usawa mahali pa kazi.
Amesema ni vyema
wakachukua fursa hii kujadiliana na
kutafakari si kwa maslahi yao tu, bali utendaji wa kazi wa kila siku na jinsi
ya kuboresha zaidi.
“Hii ni kwa
sababu tija na maslahi ni matokeo ya utendaji bora unaolenga kutoa huduma bora kwa
wananchi na kuchangia maslahi bora kwa watumishi,” amesema Naibu Waziri.
Naye Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Duwasa, Aron Joseph akizungumza kabla ya kumkaribisha
Mwenyekiti wa Bodi, amesema lengo la
mkutano huo ni kulikumbusha baraza kuhusu majukumu yao na kuwaelmisha juu sheria
na utaratibu wa uendeshaji wa baraza hilo.
Mwenyekiti
wa Bodi, Prof. Fautine Bee, alianza kwa kuwapongeza
wajumbe 63 baraza hilo la sita na
kulitaka kufanya kazi kwa ushirikiano na menejimenti pamoja na wafanyakazi wa
Duwasa. kutekeleza majukumu ambayo baraza linatakiwa lifanye.
Prof. Bee alitaja baadhi
ya maazimio waliyoafikiana kwenye mkutano huo ili waendelee kutoa huduma iliyo bora kuwa ni;
Mamlaka iendelee kutoa huduma zilizo bora, kupunguza kero kwa wananchi kuhusu
upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazingira, Kupunguza upotevu wa maji
kutoka asilimia 26 kwenda chini, na kuongeza ukusanyaji mapato.
Mengine ni,
kuhudumia wateja kwa haraka na ufanisi, kupata suluhisho la tatizo la maji
chumvi, uvunaji wa maji na kuongeza kasi ya uwekezaji.
Pia
wameahidi Duwasa kuwa mamlaka bora si
kwa Tanzania lakini kwa bara zima la Afrika.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇