Mpachila akiwa na mkewe Catherine ndani gari baada ya kukabidhiwa.
Mpachila akijiandaa kuondoka na gari lake baada ya kukabidhiwa rasmi.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Maganga akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Vodacom iliyoendesha promosheni ya Shangwe Shangwena.
Gari la Mpachila likiondoka kwenye viwanja vya Nyerere Square huku akishangiliwa
Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma.
Mkazi wa Ipagala, jijini Dodoma,William Mpachila amekabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,
Josephat Maganga zawadi ya gari aina ya Renault Kwid baada ya kushinda shindano
la Tumia M-Pesa Ushinde katika promosheni ya Shangwe Shangwena ya kuadhimisha
miaka 20 ya Vodacom Tanzania.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hiyo eneo la Nyerere
Square, jijini Dodoma, Mkuu huyo wa
Wilaya ya Dodoma, Josephat Maganga, ambaye katika hafla hiyo alimwakilisha Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge, aliipongeza vodacom kwa kutimiza azma
ya serikali ya kuzisogeza karibu kwa wananchi huduma za mawasiliano ya simu na
za kifedha kupitia M-Pesa kwa kipindi
chote cha miaka 20.
Naye Meneja wa
Vodacom Kanda ya Kati, Grace Chambua amesema katika kuadhimisha miaka 20, licha
ya kutoa punguzo 15% kwa bidhaa zao, lakini wameendesha promosheni ya Shangwe
Shangwena ya Tumia M-Pesa Ushinde kwa kutoa zawadi ya magari matano, sh.
milioni 25 kwa wateja 25 kila mmoja sh. mil 1, na kwamba zawadi zote
zimegharimu zaidi ya sh. bil. 3.
Mshindi wa gari hilo,
Mpachila ambaye ni dereva wa pick up ndogo aina ya kilikuu ameishukuru Vodacom
kwa kumpatia zawadi hiyo ambayo hakuitegemea na kwamba ataitumia kwa shughuli
zake binafsi.
Aidha, Mpachila amewawashauri vijana na wananchi kwa ujumla, kutozibeza promosheni zinazoendeshwa na Vodacom akidai ni za ukweli na ndiyo maanda yeye amefanikiwa kushinda na kutwaa gari hilo.
Mpachila licha kuwa dereva mzuri mwenye leseni, kwa furaha kubwa aliyokuwa nayo alishindwa kabisa kuendesha gari hilo, hivyo ilibidi asaidiwe kuendesha na ndugu yake kuelekea kwao Ipagala.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇