CCM Blog, Dar es Salaam
Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Tanzania kuanzia mwaka 1980 hadi mwaka1988, Jenerali David Bugozi Msuguri leo ametimiza umri wa miaka 101, sawa na Karne moja na mwaka mmoja.
Musuguri ambaye asili yake ni Mudoma mkoani Mara, ndiye aliyeongoza majeshi ya Tanzania kumfurusha Nduli Iddi Amin Dada wa Uganda mwaka 1978 baada ya kuvamia eneo la Kyaka mkoani Kagera na kulitangaza kuwa ni miliki ya Uganda.
Aliongoza Makamanda wenzake na wapiganaji chini ya Amiri Jeshi Mkuy Rais wa Kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere na kushusha kichapo kilichomfanya Idi Amini aiache ardhi ya Tanzania eneo la Kyaka na kurudi Uganda.
Kwa kuwa alizoea vitisho kwa Tanzania kwa kudai Kagera ni eneo la Uganda Majeshi ya Tanzania chini ya Jenerali Musuguri yaliamua kumchapa Amini hadi nchini mwake Uganda na katika mji wake mkuu Kampala na kumfukuza kabisa katika Ardhi ya Uganda na kwenda kuishi Uhamishoni Saudi Arabia.
Jenerali David Musuguri alizaliwa Januari 4 1920, Butiama mkoani Mara na alihufumu katika Jeshi tangu Mwaka 1942–1988
Mapambano na vita aliyoshiriki ni pamoja na Vita Kuu ya Pili ya Funia, Battle of Madagascar, Vita vya Kagera, Battle of Simba Hills na alianza kuhudumu katika Jeshi la King's of Rifles (KR), Tanganyika Rifles kabla ya kuwa Jeshi la Ulinzia Wananchi was Tanzania (JWTZ).
KWA NINI MBEZI KWA MSUGURI?
Jijini Dar es Salaam lipo eneo linaloitwa Mbezi kwa Musuguri kutokana na kuwa ndilo Makazi ya Mwamba huyu David Musuguri ambaye leo ametimiza miaka 101 ambayo ni sawa na karne moja na mwaka mmoja.
Blog ya Taifa ya CCM inatoa hongera sana kwa Jenerali Musuguri na Mungu azidi kumjaalia maisha marefu marefu zaidi na zaidi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇