MPISHI Mkuu wa Shule ya Fountain Gate Academy ya jijini Dodoma, akielezea jinsi Mkaa Mweupe unavyorahisisha mapishi ya vyakula mbalimbali tofauti na matumizi ya mkaa mweusi kuni kuni.
Mpishi huyo anasema kuwa kabla ya kuanza kutumia Mkaa Mweupe walikuwa wanatumia magunia manne hadi matano ya mkaa mweusi kwa siku ambayo gharama yake ilikuwa zaidi ya 160,000, lakini hivi sasa wanatumia viloba vinne vya mkaa mweupe ambayo gharama yake ni sh. 80,000 hivyo kuokoa zaidi ya sh 80,000.
Pia, anasema kuwa Mkaa Mweupe hautoi moshi lakini pia vipande kati 8-10 unaweza kupikia chai, wali, ugali na mbogamboga zingine bila kuzimika vilevile mabaki ya moto huo unaweza kupalia juu ya sufulia la wali ili kuivisha vizuri.
Pia unaweza kutumia vipande 7 hadi kumi kupikia maharage kilo therathini hadi arobaini kwa muda wa lisaa limoja hadi saa moja na nusu.
Ndugu mdau nakuomba uendelee kumsikiliza Mpishi huo akielezea kupitia clip hii ya video kuhusu manufaa zaidi ya Mkaa huo Mweupe...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇