Maneno ya aliekuwa Kocha wa Simba Sven “Nimeachana kwa amani na Simba ili kutafuta uwiano kati ya kazi na familia yangu, na kwa ajili ya maendeleo binafsi. Nimefanya hivyo kwa moyo mzito kwa sababu nilikuwa sehemu ya Simba na Simba ikawa sehemu yangu”.
“Ninawashukuru wachezaji wote kwa mchango wao katika mafanikio yetu na mashabiki kwa kumbukumbu nzuri. Ninawashukuru Mo Dewji na CEO Barbara kwa weledi wao na kwa kunisadia kufanya kazi yangu” Sven
“Wote walijaribu kunishawishi nibaki mpaka sekunde ya mwisho.“Siku zote nitaitakia Simba mafanikio makubwa“ aliyekuwa Kocha wa Simba” Sven
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇