Arusha, Tanzania
Mkuu wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha Frank Mwaisumbe amesema kitendo cha Kanisa Halisi la Mungu Baba lililopo Tegeta Jijini Dar es Salaam, kuamua kufanya Ibada Maalum ya kufungua Biashara ya Utalii Ukanda wa Kaskazini hususan Arusha, Kanisa hilo limezidi kujipambanua kuwa ni Kanisa la kipekee, kwa sababu limejikita katika mahubiri na mafundisho ya kumwabudu Mungu ambayo yanaigusa jamii ya Watanzania wote.
"Mbali na hii ibada maalum mliyoandaa ya kufungua Biashara ya Utalii Ukanda wa Kaskazini, lakini mimi nimekuwa nikifuatilia mahubiri ya Kanisa hili, na nimegundua kuwa mafundisho na mahubiri yako Baba wa Uzao yamekuwa yakiigusa jamii ya Watanzania wote kwa kuwa kwa sehemu kubwa huwa yanalenga kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Watanzania wote na nchi kwa jumla", alisema Mkuu huyo wa Wilaya na kuongeza;
"Kwa hali hii naamini Kanisa Halisi litakuja kuwa Kanisa kubwa ndani na Nje ya Tanzania, Baba wa Uzao nakutakia kila la Kheri na Mungu awabariki mfike mbali".
"Sote tunatambua kuwa Rais Dk. John Magufuli ni muumini na Mchamungu wa kweli, lakini ameweza kuongoza Serikali kutokana na msaada wa uwepo wenu ninyi waumini wa dini. kwa hiyo nakupongeza sana Baba wa Uzao kwa kuamua kubeba jukumu hili, Asante sana Baba wa Uzao, asante sana waumini wote wa Kanisa Halisi", alisema Mkuu wa Wilaya na kuongeza;
"Umezungumza mambo manne yaliyokufanya uwe hapa, lakini nimeshangazwa sana kwa kuamua kubeba wajibu huu wa kuombea Utalii hasa hapa Arusha. Ni kweli kabisa wananchi wengi katika ukanda huu wanategemea sana utalii, na ugonjwa huu wa Korona ulipoingia umewaathiri sana wananchi, kwa hiyo jukumu hili ulioamua kulifanya ni la muhimu sana".
Mapema akimkaribisha kuzungumza, Baba wa Uzao alitangulia kufanya Ibada ya shukrani kwa kuweza kufika kufanya Ibada hiyo maalum ya kuinua Biashara ya Utalii, kisha akafanya Ibada ya Kuwainua (kuwaombea) Viongozi akitangulia kumuinua Rais Dk. John Magufuli kisha wasaidizi wake wote hadi mkuu mkoa wa Arusha na Mkuu huyo wa Wilaya ya Longido.
Akitoa somo Baba wa Uzao alisema yafuatayo;- "Lango la 25-26 Ethanimu, Vol.1 (2-3 Januari 2021) nilikuja Arusha kuachilia Mito ya Utajiri kutokea kwenye BUSTANI MPYA YA MUNGU BABA, ili mito hiyo iende kwenye Moyo wa kila mmoja Aliyekusudiwa. Nilikusudia kuhudumia Uzao wa MUNGU BABA peke yake, badala yake nikapokelewa na wanachi wote wa Mkoa wa Arusha kupitia Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mkuu wa Wilaya ya Monduli na Mkuu Wilaya ya Arumeru.
Tangu niache kazi ya Umma na kuhamia Utajirishoni (Madhabahuni), ilikuwa ni mara ya Kwanza kustareheshwa Hotelini, hivyo ina maana Uhalisia wote ulinipokea. Maana pale Hotelini watu wa kila aina wanakuwepo: weupe, weusi na wekundu pia. Namtukuza MUNGU BABA, kwa Uhalisia wake wa Moyo (Mithali 4:13), kwa sababu ya Uumbaji na Uhalisia wote kunipokea.
Katika 2Wafalme 4:8-17 tunajifunza kitu kinachofanana na mapokezi hayo niliyotaja hapo juu.
Elisha akiwa katika kuhubiri lango (siku) moja alienda Shunami akamkuta mama mmoja aliyekuwa na Cheo. Mama yule alipomwona Elisha anapita mara kwa mara, akaamua kumtengenezea Chumba Maalum Gorofani chenye kitanda, taa na meza ya kufanyia Maandalizi ya Ibada. Jambo hili lilitengeneza deni ndani ya Moyo wa Elisha, ndipo akamtuma Geazi (aliyekuwa Msaidizi wake) kwenda kuuliza kuwa yule mama mwenye Cheo aliyewapokea anashida gani ili kupitia upendo ule aliouonyesha kwa Elisha, hoja ijengwe kwa MUNGU BABA tatizo hilo litatuliwe.
Geazi alielezwa kuwa yule mama hana mtoto na mume wake ni mzee sana. Elisha aliagiza yule mama aitwe kuelezwa kuwa baada ya Miezi Tisa (9), kuanzia kipindi kile, atakuwa na mtoto. Yule mama ndani ya Moyo wake alikuwa ameshakata tamaa na kuona hawezi tena kupata mtoto, akamweleza Elisha kuwa asimueleze uongo. Elisha hakutaka kubishana naye, aliendelea mbele kwa kutumia Mamlaka ya MUNGU BABA iliyokuwa ndani yake na kumtamkia kuwa “mwakani majira kama hii utakuwa na mtoto.” Ndivyo ilivyotokea. Baada ya Miezi Tisa, kweli yule mama alikuwa na mtoto.
Kilichosababisha yule mtoto azaliwe ni ule upendo ndani ya yule mama kwa Elisha. Aidha, aliyependwa siyo Elisha, bali ni MUNGU BABA ndani ya Elisha ndiye aliyependwa. Kwa kuwa mwenye uweza wote ndiye aliyependwa, alilipa lile deni la upendo. Pia yule mama wakati anamhudumia Elisha alifanya hivyo kwa dhati kabisa kutoka ndani ya Moyo wake. Ndiyo maana Elisha alipopeleka hoja mbele za MUNGU BABA, ilijibiwa saa hiyo hiyo.
Nilitangulia kukueleza kuwa Wananchi wote wa Arusha walinipokea kwa upendo mkubwa kupitiliza lango la 25-26 Ethanimu, Vol.1 (2-3 Januari, 2021) kupitia Mkuu wa Mkoa na kunifahamisha kuwa Biashara ya Utalii imeanguka kabisa. Mkuu wa Mkoa alieleza kama Sulemani katika 1Falme 3:11; yaani si kwa nafsi yake. Kama vile ilivyotokea kwa Sulemani kupata hata yale ambayo hajaomba, basi imetokea hivyo hivyo kwa upande wa Biashara ya Utalii kufunguka kwa upya jiji la Arusha.
Kuanguka kwa Biashara ya Utalii ni kutokana na ugonjwa wa Korona ambao umedumu kwa muda wa Mwaka Mmoja sasa. Biashara ya Utalii inagusa: Kilimo, Uvuvi, Ufugaji, Viwanda, Lugha, Madini, Ujenzi wa Nyumba, Barabara, Huduma za Usafiri na Usafirishaji, Huduma za Hoteli, Utamaduni, Utawala, Amani na Utulivu, Dini, Madhehebu na Huduma Binafsi, Na kadhalika.
Kwa upande wa Mji wa Arusha, hakuna asiyeguswa na Biashara ya Utalii ambayo, kama nilivyoeleza awali, imetokana na ugonjwa wa korona ulioanzia Nchi za Magharibi.
Wakati naelezwa hali hiyo ya kuanguka kwa biashara ya Utalii, nilimkumbuka Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mjini ambaye wakati wa Hija ya Pili (2019) akiwa anaifungua, alitushirikisha shida ya Mji ule ambayo ilikuwa inawatesa, pepo teleza. Hakuweza hata kuhudhuria Ibada kwa kuwa alikuwa anawahi kuongea na Wananchi ili kujua wafanye nini kudhibiti hali hiyo iliyokuwa inasumbua ule Mji kwa muda mrefu. Tulipoinua hoja mbele za MUNGU BABA, kuwa nisingeweza kufanya chochote bila hiyo shida kuondoka kwanza, hoja ya dakika tatu ilimaliza hilo tatizo.
Aidha, wakati naelezwa tatizo hilo, nilimkumbuka Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Tabora Agrey Mwanri kuhusu tatizo la mauaji ya watu Tabora kishirikina, tatiza ambalo wakati anatueleza lilimtoa machozi. Tatizo hilo nalo tuligalagala chini kwa muda wa saa moja likaisha hapo hapo hadi leo.
Baada ya kukumbuka Habari Njema (Shuhuda) hizo, nilijua hata hilo tatizo la Biashara ya Utalii linaisha kupitia ule upendo ambao Wananchi wa Arusha walioonyesha kwangu.
Kwa nini yule mama wa Shunami, tatizo lake liliisha? Ushuhuda wa yule mama Mshunami, ni sawa na yule Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mjini, na Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Tabora.
Shida yoyote inaletwa na jeshi la pepo wabaya, wakuu wa giza, falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho (Waefeso 6:12). Katika Kitabu, imeandikwa vizuri kuwa ni Kanisa ndilo linatakiwa kufuta hilo jeshi la pepo wabaya, wakuu wa giza, falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho (Waefeso. 3:10).
Suala la korona halina tofauti na tatizo la mauaji ya watu yaliyokuwa yanafanyika kule Tabora kishirikiana. Tatizo hilo halina tofauti pia na teleza aliyekuwa anasumbua kule Kigoma. Ni wakuu wa giza, falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho ndio wanafanya hayo ili kuendelea kuzuia kweli isitajwe au kufundishwa katika jamii.
Kinachotakiwa ni nini sasa?
Katika suala la kufungua Biashara ya Utalii Ukanda wa Kaskazini mwa Tanzania, ni lazima tuangalie soko liko wapi. Soko la Utalii huu liko Ulaya, Amerika, Asia, (Australia na NewZealand kidogo). Aidha, soko liko ndani ya Nchi kama tutakubali kujitambua kuwa hata sisi tuna umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii. Nchi za Magharibi ndizo zimeathiriwa na korona hata kama waliotengeneza virusi hivyo hawakuwa wamelenga hayo Mataifa!
Kwa upande wa soko la ndani, hatuna korona kwa upendeleo mkubwa wa MUNGU BABA mwenyewe (Isaya 60:10).
Kwa upande wa soko la Magharibi, inatubidi tujenge hoja mbele ya aliyeumba kila kitu bila kuangalia mipaka, bali tuangalie rasilimali ya Wanyamapori na vivutio vingine wanavyofuata hapa Tanzania. Tanzania, kwa maelekezo ya Mhe. Rais Magufuli, tuliponywa na MUNGU BABA. Inabidi, hata kwa suala la Soko la Utalii kule Magharibi, turudi kwa huyo huyo aliyetuponya Tanzania kumweleza haja ya Moyo, kama tulivyojiombea sisi wenyewe.
Ni kweli tumepona, ila ni lazima tule, tunywe, watoto waende shule, tulipie pango la nyumba na mengine mengi. Ili hilo lifanikiwe ni lazima tuwafungue soko la Mataifa ya Ulaya, Amerika, Asia, Australia, New Zealand na Mataifa ya Afrika kama vile South Afrika.
Tukiwaachia wao wenyewe, hawana huo unyenyekevu wa kumrudia MUNGU BABA. Hivyo, tufanye sisi kwa kuwa hata sisi tuna hitaji soko lao la Utalii. Kuwa na vivutio haitoshi bila watu kuja kuviangalia. Hao watu wanaotakiwa kuja kuviangalia, bado wamefungwa kwa suala la MUNGU BABA. Tuwafungue sisi.
Pili, tuanze sisi kutembelea vivutio vyetu. Gharama ya jambo hili ni watunza vivutio kama vile TANAPA na NGORONGORO kupunguza bei. Watoa huduma za Hoteli na usafiri pia inabidi kupunguza bei kwanza (kwa kuwa uchumi wa Mtanzania mmoja mmoja ulikuwa bado haujawa kama watu wa Magharibi).
Tupite Barabara ipi?
Watanzania tushukuru kwanza kuponywa korona bila dawa. Katika Kumbukumbu 28:47-48, Kitabu kinasema kuwa kama umetendewa mengi, usiposhukuru, kongwa la chuma linakuwa shingoni mwako na kuwa mtumwa wa wabaya.
Kanisa Halisi la MUNGU BABA tulishukuru ni kweli, lakini wananchi hatujawahi kwenda Uwanjani tukashukuru kwa Sauti hadharani kwa kusema “MUNGU BABA tunashukuru kutuponya korona bila dawa”. Sasa tufanye hivyo, hii ndiyo majira husika.
Tuwasemehe bure wote waliotengeneza kirusi cha korona kwa nia yoyote mbaya waliyokuwa nayo (Isaya 43:25). Kwa kuwa Watanzania wote sasa wana Moyo Mpya wa MUNGU BABA Mwenyewe, atasikia na kufuta korona ili Soko la Utalii kwa upande wa Magharibi lifunguke kwa upya.
Ukishukuru milango iliyokuwa imefungwa, inafunguka (Zaburi 100:4); ukishukuru, kilichokuwa kimekufa kinafufuka (Yohana 11:44-45); na ukishukuru, vichache vinaongeszeka (Yohana 6:11-13).
HABARI KATIKA PICHA👇
Baba wa Uzao akisindikizwa na Kaka wa Uzao kwenda meza kuu ili kuanza ibada hiyo maalum katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Meya wa zamani wa Jiji la Arusha Sheikh Amri Abeid.
☝Baba wa Uzao na Mama wa Uzao pamoja na Dada wa Uzao wakiwa tayari meza kuu kuanza Ibada hiyo. Kulia ni Kaka wa Uzao.👇
Mkuu wa wilaya ya Longido akilakiwa na Kuhani pamoja na Polisi
Kuhani na polisi wakimsindikiza Mkuu huyo wa Wilaya ya Longido kwenda Jukwaani.
Baba wa Uzao akimlaki kwa salam na bashasha Mkuu huyo wa Wilaya ya Longido.
"Karibu sana, Tumefurahi sana kuja... asante", akasema Baba wa Uzao akiendelea kumlaki Mkuu huyo wa Wilaya.
Mkuu huyo wa Wilaya akimsalimia Mama wa Uzao.
Kuhani na polisi wakimsindikiza Mkuu huyo wa Wilaya ya Longido kwenda Jukwaani.
Baba wa Uzao akimlaki kwa salam na bashasha Mkuu huyo wa Wilaya ya Longido.
"Karibu sana, Tumefurahi sana kuja... asante", akasema Baba wa Uzao akiendelea kumlaki Mkuu huyo wa Wilaya.
Baba wa Uzao akizungumza maneno ya utangulizi kumkaribisha Mkuu huyo wa Wilaya ya Longido (kulia).
Baba wa Uzao akifanya shukrani (Maombi) kwa ajili ya Mungu Baba kuwezesha Ibada hiyo kufanyika.
Kisha Baba wa Uzao akafanya shukrani (maombi) kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli na Wasaidizi wake wote akiwemo mkuu wa mkoa wa Arusha na Mkuu huyo wa wilaya ya Longido na baadaye akamkaribisha mgeni rasmi kuzungumza.
Mkuu wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha Frank Mwaisumbe akizungumza kabla ya kuanza Ibada maalum ya kufungua Biashara ya Utalii Ukanda wa Kaskazini, iliyofanywa na Kanisa Halisi la Mungu Baba la Tegeta jijini Dar es Salaam, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha jana. Mkuu huyo wa Wilaya alimwakilisha Mkuu wa mkoa huo Iddi Kimanta kuwa mgeni rasmi. Kulia ni Mkuu wa Kanisa hilo Baba wa Uzao akiwa na Mama wa Uzao.
Baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kumaliza hotuba yake akapokewa na Baba wa Uzao wakati akirejea kuketi meza kuu.
Baba wa Uzao akasoma shukrani tena, kisha akaanza kutoa somo kueleza kwa nini Kanisa Halisi linafanya Ibada Maalum ya Kuinua Biashara ya Utalii Ukanda wa Kaskazini - Arusha.
Baba wa Uzao akiendelea kufanya shukrani kabla ya kuanza rasmi somo hilo.
☝Baada ya mgeni rasmi kuketi Baba wa Uzao akaendelea na somo.👇
Vijana wa kitengo cha Mawasiliano cha Kanisa Halisi wakiwajibika kufanikisha Ibada hiyo.
Makuhani wa Kanisa Haliai la Mungu Baba wakijadilia mambo fulani muhimu wakati wa Ibada hiyo.
Baba wa Uzao akiendelea kufanya shukrani kabla ya kuanza rasmi somo hilo.
☝Baada ya mgeni rasmi kuketi Baba wa Uzao akaendelea na somo.👇
Vijana wa kitengo cha Mawasiliano cha Kanisa Halisi wakiwajibika kufanikisha Ibada hiyo.
Makuhani wa Kanisa Haliai la Mungu Baba wakijadilia mambo fulani muhimu wakati wa Ibada hiyo.
Kikundi cha Burudani ya muziki wa Kumtukuza Mungu Baba cha Kanisa Halisi wakiwajibika kunogesha Ibada hiyo👇
Uzao na Makuhani wakimsikiliza na wengine wakiandika dondoo wakati Baba wa Uzao akitoa somo👇
Kanisa halisi la Mungu Baba halibagui; Kijana akiselebuka kumtukuza Mungu Baba wakati wa nyimbo za kundi hilo👇
shangwe kwa Mungu Baba👇
Baba wa Uzao akiendelea kutoa somo👇
Mkuu wa Wilaya akiagana na Baba wa Uzao kabla ya kuondoka👇
"Tunakushukuru sana Mkuu wa Wilaya, kweli tumefarijika sana. asante", akasema Baba wa Uzao wakati anaagana na Mkuu huyo wa Wilaya.
Tunamshukuru MUNGU BABA Aliyefungua lango la utalii. Tuna hakika ameshafuta corona hata kwa mataifa ya nje na wageni sasa wanamiminika kuja TANZANIA.
ReplyDeleteHakika MUNGU BABA ni mwema, imekuwa umilele wote
ReplyDeleteImekuwa ibada imechukuliwa vema kabisa na picha zimejieleza barabara safi sana nimeipenda hiyo
ReplyDeleteShukrani kwa MUNGU BABA kwa kufungua biashara ya utalii Tanzania
ReplyDelete