LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 9, 2021

DK. MAHENGE AAGIZA KILA MTUMISHI KUPANDA MITI KUMI KILA WIKI KUIFANYA DODOMA YA KIJANI

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge akishiriki kupanda miti eneo la Medeli jijini Dodoma leo Desemba 9,2021. 


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Josephat Maganga akishiriki kupanda miti katika eneo hilo.

Dkt. Mahenge akizungumza baada ya kushiriki kupana miti eneo la Medeli.

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma,  Joseph Mafulu akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Idara ya Mazingira wa Jiji  hilo, Dickson Kimaro kuelezea mipango ya jiji kuhusu upandaji miti.
Dkt. Binilith Mahenge (kulia), akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Josephat Manganga pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru (kushoto).
Baadhi ya walioshiriki kupanda miti kutoka taasisi mbalimbali zilizoalikwa 





Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma,  Mafuru akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma walioshiriki kupanda miti.

Mafuru akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa UDOM pamoja na baadhi waliotoka kwenye taasisi zilizoalikwa kushiriki zoezi la upandaji miti. Picha zote na Richard Mwaikenda


Na Richard Mwaikenda, Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge ameagiza kila Mtumishi katika Halmashauri zote za wilaya kupangiwa kupanda miti 10 kwa wiki ili kutunza mazingira na kuifanya Dodoma kuwa ya Kijani.

Agizo hilo amelitoa leo baada ya kushiriki upandaji miti eneo la Medeli jijini Dodoma ambapo yeye binafsi amepanda miti 22  na kutaka iwekewe alama ya jina lake kwa kumbukumbu  zaidi.


Dkt. Mahenge, ameagiza watumishi ambao ahawakushiriki katika zoezi la upandaji  miti leo, wiki ijayo inatakiwa wapande miti 20 kufidia ambayo hawakupanda ili waende sawa wenzao walioshiriki.

 

“Hili tutaliingiza kwenye utaratibu wa nidhamu ya kikazi, hivyo wale ambao hawakuja leo basi watapanda miti kumi ya wiki hii na 10 ya wiki ijayo,” ameagiza Dkt. Mahenge.

 

Mkuu wa Mkoa alishangaa kuona idadi ndogo ya watumishi waliofika inayozidiwa na watu walioalikwa kutoka taasisi zingine , ambapo alisema kwa sasa zitatengezwa sheria ndogo za nidhamu ya kazi kuwabana.


Dkt. Mahenge aliutaka uongozi wa Jiji la Dodoma kuainisha maeneo na kuyagawa kwa taasisi mbalimbali pamoja na watumishi wa serikali kwa ajili ya kupanda miti na kuweka alama ya taasisi na mtumishi anayelitunza.


Alisema kuwa utaratibu huo ufanywe pia kwa halmashauri zote za mkoa huo ili kutimiza azma ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.

 

Amesema kuwa wakifanikiwa kutekeleza hilo,  itakuwa ni rahisi kuvuka hata lengo la kila Halmashauri kupanda miti milioni 1.5 lililowekwa na Makamu wa Rais mwaka 2006 ambalo hadi sasa halijawahi fikiwa.


Aidha, Dkt Mahenge  amesema kuwa hakuna mtu mwingine atakayeifanya Dodoma kuwa ya kijani bali ni wananchi wa Dodoma wakiongozwa vyema na viongozi wao mahali walipo.

 

Awali, akielezea mipango ya upandaji miti katika Jiji la Dodoma, Mkuu wa Idara ya Mazingira wa Jiji hilo, Dickson Kimaro amesema kuwa hadi sasa imepandwa miti 150,000 na kwamba kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), wameotesha miche milioni 2 ambayo hugawiwa bure kwa wananchi.


Pia, amesema kuwa wameweka utaratibu wa kila mkazi wa Jiji hilo kuhakikisha anapanda miti mitano katika mazingira yanayomzunguka kwa kugawiwa miche bure, lakini pia wameweka sheria kwa kila kibali kinachotolewa cha ujenzi lazima mhusika  apande miti kabla ya kuanza ujenzi.


Kimario amesema kuwa ili jiji lizidi kuwa la kijani wamekubaliana na baadhi ya taasisi zikiwemo za kibenki kupanda miti kando ya barabara zinazoingia katika Jiji hilo na tayari wameanza katika baadhi ya barabara.


Alitaja baadhi ya taasisi  zilizoshiriki katika kazi ya upandaji miti leo kuwa ni; Ofisi ya Mkoa, Wilaya ya Dodoma,  Chuo Kikuu cha Dodoma, Wakala wa Misitu (TFS), Green Waste, Skauti, mabenki, Tanesco na Mzakwe.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages