Mbunge wa Jimbo la Buyungu Aloyce Kamamba (Wanne kutokana kulia) akiwa na Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kakonko wakati wakikagua miradi katika jimbo hilo.
Na Jastin Cosmas, Kakonko
Wazazi na walezi wilayani Kakonko mkoani Kigoma wamehimizwa kuhakiksha watoto walio faulu mtihani wa darasa la saba wanaanza masomo wakiwa na mahitaji yote shule za sekondari zinapofunguliwa
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kakonko Saamoja wakati kamati ya siasa ya wilaya ikikagua miradi mabalimbali hapa wilayani Kakonko ambapo amesisitiza suala hilo
Kwa upande wake Mbunge wa Buyungu Aloyce Kamamba amewataka Watendaji wa Kata kuwabaini Wazazi ambao wana waajiri watoto wanaopaswa kuwa shule kitendo ambacho kinarudisha nyuma elimu hivyo ametowa mwito kuhakikisha watoto walio faulu wanapelekwa shule.
Wakati huohuo Mbunge huyo ametoa kilo 100 za mchele na mabati yenye thamani ya sh. milioni 1.5 katika shule ya Sekondari Mugunzu iliyopo katika tarafa ya Kasanda ili kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Aidha Katibu tarafa wa tarafa ya Kasanda Amani Kanguye akimwakilisha Mkuu wa We ya Kakonko amesema kuwa mzazi au mlezi atakae kaidi kumpeleka mtoto shule hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇