MBUNGE wa
Viti Maalumu Mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakang’ata ametoa misaada mbalimbali ya
saruji pamoja na madawati mkoani humo.
Mwakang’ata
ametoa mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya sh. Milioni 12 kwa shule 10 za
msingi zilizofanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba na shule 10 zenye
mahitaji maalumu katika manispaa ya Sumbawanga.Kila shule inapata mifuko 10.
Shule zilizonufaika ni; Mwenge A, Kantalama Mazoezi, Mapinduzi, Chemchem, Lukewile, Utengule, Kiwelu, Mwenge B, Kizwite na Molo.
Katika hafla
hiyo iliyofanyika hivi karibuni mjini Sumbawanga, mbunge huyo alitoa pia zawadi
ya vyeti, katoni za sukari na zawadi
zinginezo kwa walimu ambao shule zilifanya vizuri.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Mbunge Mwakang’ata, alisema ameamua kufanya hivyo ikiwa ni shukrani kwa
wananchi waliomwezesha kushika wadhifa huo, lakini pia kuunga mkono juhudi za
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kuhusu elimu bure ambayo
imefanya wanafunzi wengi kupata elimu.
Madawati
50 yenye thamani ya sh. Milioni 3.5 yalikabidhiwa kwa Shule ya
Msingi Manzitiswe iliyopo Manispaa ya Sumbawanga.
Akipokea
madawati hayo Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Lasko Manase alisema yeye na wajumbe
wa kamati ya shule, wameupokea msaada
huo kwa furaha kubwa kwani umepunguza kwa kiasi kikubwa upungufu wa madawati
shuleni hapo.
Manase alisema
kuwa kabla ya ujio wa madawati hayo, shule hiyo ilikuwa na upungufu wa madawati
185, hivyo kwa sasa baada ya kupatikana madawati hayo 50, upungufu utakuwa
madawati 135. Madawati hayo yamegawanywa kwenye vyumba viwili vya madarasa.
Mwalimu
Manase amewaomba wadau wengine akiwemo mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aishi
Hillary na wabunge wengine kuunga mkono juhudi za Mwakang’ata kwa kutoa msaada
wa mabawati yaliyobakia.
Naye Afisa
Elimu Msaidizi wa Manispaa ya Sumbawanga, Graseana Killenga alimshukuru sana
Munge Mwakang’ata kuwapatia msaada huo
na kuulinganisha kama lulu na kwamba saruji hiyo itasaidia sana kupunguza uhaba
wa matundu ya vyoo na kusaidia ujenzi wa baadhi ya vyumba vya madarasa katika
shule hizo kumi.
Ndugu mdau ukitaka kujua zaidi yaliyojiri katika hafla hiyo basi nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video...
IMEANDALIWA NA;
RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI LOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇