LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 1, 2021

ASKOFU CHANDE AMFANANISHA RAIS MAGUFULI NA NABII MUSSA, KUITOKOMEZA CORONA NCHINI+VIDEO

Askofu Evance Chande wa Kanisa la EAGT Nazaret, Ipagala, jijini Dodoma, akiwaombea waumini wa kanisa hilo wakati wa ibada ya kuukaribisha mwaka mpya 2021 na kuliombea Taifa amani na utulivu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA.
Askofu Chande akisisitiza umuhimu wa kuilinda amani ya nchi.
Kwaya ikitumbuiza wakati wa maombi hayo.
Waumini wakisikiliza kwa makini mahubiri ya Askofu Chande.


Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma.

RAIS wa Jamhuri ya Tanzania, Dk. John Magufuli amefananishwa na Nabii Mussa aliyewavusha wana Israel kutoka nchi ya utumwani Misri kwenda Kanani nchi ya ahadi, kwa kitendo chake cha kuwavusha salama watanzania dhidi ya janga la Corona kwa kumuomba Mungu.

Kauli hiyo, imetolewa na Askofu Evance Chande wa Kanisa la EAGT Nazaret, Dodoma, wakati wa ibada ya kuukaribisha mwaka mpya  wa 2021, ambayo ilikuwa maalumu ya kuwaombea watu wa kada mbalimbali pamoja  na kuliombea Taifa kuwa la amani na utulivu.

Askofu Chande anasema anamfananisha Rais Magufuli  mcha Mungu na Nabii Mussa, kwa  uamuzi wake wakati Corona ilipopamba moto kuwatoa hofu watanzania kuwa ugonjwa huo ni kitu kidogo utatoweka tu na kuwaomba viongozi wa dini kufunga siku tatu kuliombea Taifa  kwa Mungu kuutokomeza ugonjwa huo, maombi ambayo yamejibiwa na hivi sasa Tanzania hakuna Corona.

Mdau nisikumalizie uhondo, bali nakuomba uendelee kumsikiliza Askofu Chande akielezea juu ya hilo kupitia kwenye Clip hii ya Video….


No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages