NA DENIS MLOWE, IRINGA
MKURUGENZI Mkuu wa TAKUKURU nchini, Brigedia Jenerali John Mbungo ametoa siku 14 kwa wakandarasi wa makampuni 16 waliokuwa wanaotekeleza miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) nchini kuhakikisha wanakabidhi vifaa ghafi kwa tanesco kutokana na mikataba waliyofikiana.
Akizungumza wakati wa kuwakabidhi shirika la umeme nchini (TANESCO) vifaa ghafi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 1. 2 vilivyookolewa kutoka kwa mmoja ya wakandarasi ,Brigedia Jenerali Mbungo alisema kuwa makampuni 16 yanatakiwa kukabidhi vifaa ghafi hivyo kuanzia Leo kwa mujibu wa mikataba yao.
Alisema kuwa licha ya kukumbushwa mara kwa mara kufanya urejeshaji huo na kupewa NOTISI ya kufanya hivyo mwaka 2017 wameshindwa kukabidhi vifaa ghafi hivyo kwa tanesco hivyo siku 14 kuanzia Leo wahakikishe wanakabidhi.
Alisema kuwa Vifaa ghafl vilivyokabidhiwa kwa shirika hilo mkoa wa Iringa vimetokana na Operesheni ya uchunguzi wa Miradi ya REA II iliyofanyika katika mkoa wa Iringa.
Alivitaja Vifaa ghafl hivyo ni pamoja na Transfoma 34 zenye ukubwa tofauti, Mita za LUKU 1,458 na vifaa vyake, Nyaya zenye urefu wa km 70.8 pamoja na Vifaa 3O vya umeme (Ready boards) vya aina tofauti tofauti vyote vikiwa na thamani ya shilingi Bilioni Moja, Milioni Mia Mbili Kumi na Sita, Laki Nane na Arobaini, Mia Tatu na Sitini(1,216,840,360.)
Brigedia Jenerali Mbungo aliyataja makapuni hayo yanayotakiwa kurejesha vifaa ghafi na kupelekewa notisi na REA tangu mwaka 2017 lakini bado hawajawasilisha vifaa ghafi hivyo katika ofisi za TANESCO
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇