Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusuf Singo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania jijini Dodoma.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
MKURUGENZI wa Michezo
wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusuf Singo, amewataka
viongozi wa vyama vya michezo nchini wanaokiuka katiba zao na kudidimiza
michezo wajiondoe wenyewe ama waondolewe.
Singo ameyasema hayo alipokaribishwa kuzungumza wakati wa
ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC),
Dodoma Hoteli jijini Dodoma leo Desemba
12, 2020.
Amesema wapo viongozi wa vyama wanaofanya kwa makusudi
kuzikiuka katika zao kwa kutofanya chaguzi na kutoendeleza michezo, hivyo wanatakiwa
kujiondoa ama kuondolewa ili wapatikane viongozi wenye moyo na uwezo wa
kuendeleza michezo nchini.
Singo, amesema kauli aliyoitoa Rauis wa Tanzania, Dk. John
Magufuli wakati anawaapisha mawaziri na
manaibu waziri Ikulu ya Chamwino, kuwa hapendi tena kusikia timu za Taifa
kufungwa fungwa magoli 10, hakumaanisha kwa mchezo wa soka tu, bali michezo
yote nchini.
Alisema wajue kwamba vyeo walivyo navyo si vya kwao bali
wanawawakilisha wananchi, hivyo kinachotakiwa kwao kufanya kazi kwa bidi kuhakikisha wanaiendeleza michezo ili timu za Taifa ziwe
zinapata ushindi na kuwafurahisha Watanzania.
Singo, amesema wiki ijayo wameandaa Kongamano la wadau wa michezo wakaojadili
namna ya kuinua hadhi ya michezo nchini. Mgeni rasmi katika Kongamano hilo
anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent
Bashungwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇