LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 1, 2020

SIKU YA UKIMWI DUNIANI ILIVYOADHIMISHWA MKOA WA DODOMA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Maduka Kessy akihutubia ka niaba ya Mkuu wa Mkoa, Dk. Binilith Mahenge wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma  Desemba 1, 2020. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma, Sharifa Nabalang'anya na Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu wa maandalizi ya maadhimisho hayo, Clispin Kapinga hayo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma, Sharifa Nabalang'anya akizungumza kuhusu hatua ambazo idara hiyo inachukua kupambana na janga hilo la Ukimwi.

 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Maduka Kessy ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa, Dk. Binilith Mahenge akikabidhi msaada wa pikipiki kwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Wanaoishi na Viruzi vya Ukimwi (NACOPHA) Konga ya Dodoma, Dorah Mwaluko kwa ajili ya kusaidia shughuli za Konga hiyo. Pikipiki hiyo imetolewa msaada na Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani. Wa pili kulia ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma, Sharifa Nabalang'anya  aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Jiji hilo.

Bibi Milika Mwita mkazi wa Chelela Jijini Dodoma akifurahia jambo wakati watoto wakicheza sarakasi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani
 ambayo kimkoa yalifanyika kwenye viwanja vya Nyerere  Square jijini Dodoma jana.  Bibi huyo ambaye haujui sahihi umri wake, alipoulizwa  alisema ana umri wa miaka tisa (9). PICHA NA RICHARD MWAIKENDA

 Mtoto Telufena Aloyce (17), akielezea kwa huzuni jinsi alivyoambiwa na mamake mzazi kuwa alimzaa akiwa na VVU na namna anavyopambana na maisha yake ya kila siku kwa kuuza nguo za mitumba jijini Dodoma.

Mratibu wa Huduma za Ukimwi Mkoa wa Dodoma, Dk. Abow Ahmed akisoma taarifa ya jinsi wanavyopambana kutokomeza maambukizi ya Ukimwi katika Mkoa huo ambao hivi sasa ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa maambukizi ya Ukimwi nchini.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Maduka Kessy ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa, Dk. Binilith Mahenge akikabidhi zawadi ya mbuzi baada ya kushinda katika mashindano ya mpira yaliyoandaliwa na kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Maduka Kessy ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa, Dk. Binilith Mahenge akikabidhi zawadi ya  mbuzi kwa  
timu ya Nacopha Konga ya Dodoma kwa washindi katika mchezo wa kuvuta kamba.
Wanafunzi wakisikiliza kwa makini wakati Katibu Tawala akihutubia kuhusu vijana kujiepusha na maambukizi ya Ukimwi.


Baadhi ya wafanyabiashara wakiuza bidhaa zao wakati wa maadhimisho hayo

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Maduka Kessy, akiondoka baada ya kuhitimisha maadhimisho hayo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages