LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 23, 2020

NAMUNGO FC WANG'ARA AFRIKA, WAICHAPA AL HILAL OBAYED YA SUDAN 2-0

 MABAO ya Sixtus Sabilo dakika ya 14 na Stephen Sey dakika ya 31 yameipa Namungo FC ushindi wa 2-0 dhidi ya Al Hilal Obayed ya Sudan jioni ya leo katika mchezo wa kwanza Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika.

Sasa Namungo FC itatakiwa kwenda kulazimisha sare ugenini au kufungwa si kwa zaidi ya tofauti ya bao moja ili kusonga mbele, ambako watamenyana na moja ya timu zitakazotolewa Ligi ya Mabingwa kuwania kucheza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho.
Kama ilivyo katika Ligi ya Mabingwa, Hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho huhusisha pia timu 16 zinazogawanywa kwenye makundi manne.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages