LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 9, 2020

NAIBU KATIBU MKUU DK. YOHAZI AKAGUA UUNGANISHAJI WA MKONGO WA TAIFA HOSPITALI YA UHURU


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iliyokuwa Sekta ya Mawasiliano,
 Dk. Jim Yohazi (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Ujenzi wa Hospitali ya Uhuru kutoka Suma JKT, Luteni Hafidh Maulid , alipokwenda kukagua maendeleo ya uwekaji mifumo ya mawasiliano iatakayounganishwa na mkongo wa Taifa katika Hospitali hiyo Desemba 8, 2020.
Mfumo huo utarahisisha mawasiliano ya simu na data hospitalini hapo. Kulia ni Meneja wa Kampuni ya Simu ya TTCL Mkoa wa Dodoma, Simon Marwa.  PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Dk. Yohazi akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa TTCL Mkoa wa  Dodoma, Simon Marwa  kuhusu uwekaji wa nyaya za mawasiliano za Mkongo wa Taifa hospitalini hapo. Dk. Yonazi ameiagiza TTCL  kukamilisha haraka uwekaji mifumo ya mawasiliano ili ianze kufanya kazi kabla ya hospitali hiyo kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto wa Wilaya ya Chamwino, Dodoma, Neema Mlula akielezea  jinsi miundombinu ya mawasiliano itakavyosaidia kurahisisha kazi za utoaji huduma hospitalini hapo.


Dk Yohazi na timu yake wakiiingia ndani ya hospitali ya Uhuru kukagua utandazaji wa mifumo ya mawasiliano ili iwe imekamilika kabla ya hospitali hiyo kuanza rasmi kufanya kazi.
Dk. Yohazi akiangalia  utandazaji wa nyaya za mawasiliano
Dk. Yohazi akiongozwa na Msimamizi wa ujenzi wa Hospitali hiyo kutoka Suma JKT, Luteni Maulid  kukagua mifumo ya mawasiliano
Dk. Yohazi na timu yake wakiwa ndani ya hospitali hiyo kukagua mifumo hiyo.
Wakiwa chumba cha maabara
Moja ya vyumba kikipakwa rangi
Ujenzi wa hospitali hiyo ukiwa katika hatua za mwisho
Wakiwa katika moja ya vyumba ambavyo uwekaji mifumo ya mawasiliano ukiendelea

Meneja wa TTCL Mkoa wa Dodoma, Simon Marwa (kulia) akimuonesha eneo ambapo nyaya za mawasiliano ZA Mkongo wa Taifa zitaingilia katika hospitali hiyo.
Nyaya za mawasiliano zikiandaliwa kwa ajili ya kutandazwa katika hospitali hiyo




Jengo la Hospitali ya Uhuru

Na Faraja Mpina  (WMTH)

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iliyokuwa Sekta ya Mawasiliano, Dkt Jim Yonazi ametembelea na kukagua hatua iliyofikiwa ya  ujenzi wa miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika hospitali ya Uhuru inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, jijini Dodoma

Dkt Yonazi amekagua Ujenzi wa wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, vyumba maalumu ambavyo mifumo ya TEHAMA itafungwa na kuunganishwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano pamoja na  upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya sauti na data ikiwemo mitandao ya simu za mkononi

Dkt. Yonazi amesema kuwa lengo la kufanya ukaguzi huo ni kuhakikisha kuwa huduma bora za mawasiliano katika hospitali hiyo zinapatikana na zinazingatia  matumizi ya kisasa ya TEHAMA

“Jukumu letu la msingi ni kuwezesha sekta mbalimbali kutumia TEHAMA ikiwemo Sekta ya Afya, lengo ni kuhakikisha Sekta ya Afya inatumia TEHAMA katika kutoa huduma zake kwa wananchi ikiwemo elimu ya afya kwa njia ya mtandao”, amesisitiza Dkt Yonazi

Naye Meneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dodoma, Simon Marwa amesema kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo umefikia kiwango cha asilimia 60 na utakamilika na kuwa tayari kutumika mara hospitali hiyo itakapoanza kutoa huduma.

Katika hatua nyingine Marwa amesema kuwa TTCL inajipanga kutekeleza agizo la Dkt. Yonazi la kuhakikisha huduma za intaneti zinapatikana kwa wananchi watakaofika katika hospitali hiyo pamoja huduma za kuweka na kutoa pesa mtandaoni kwa kutumia T-Pesa

Aidha, Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa Wilaya ya Chamwino, Neema Mlula amesema kuwa kuwekwa kwa miundombinu hiyo na mifumo ya TEHAMA katika hospitali hiyo kutawezesha utoaji wa huduma za afya, kukusanya takwimu na kuhifadhi kumbukumbu za wagonjwa

Ameongeza kuwa, mifumo ya TEHAMA itaunganishwa kwenye  vitengo nane vya hospitali hiyo ili kufanikisha utoaji wa huduma bora na kwa wakati, huku akivitaja vitengo hivyo kuwa ni wagonjwa wa nje, idara ya mionzi, maabara, kitengo cha dawa,idara ya macho, idara ya afya ya kinywa na meno, idara ya utawala na idara ya afya ya uzazi na mtoto.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages