Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Gulam Rashid akizungumza wakati wa ufunguzi
wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa kamati hiyo, katika ukumbi wa Dodoma Hotel,
jijini Dodoma Desemba 12, 2020. Gulam alikuwa mgeni rasmi katika mkutano
huo wa kuchagua viongozi watakaoongoza kwa miaka minne hadi 2024.
Katibu Mkuu wa TOC,Filbert Bayi akitoa maneno ya utangulizi wakati wa ufunguzi wa mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa TOC. |
Rais wa TOC, Gulam,akiwa na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya kamati hiyo
Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Yusufu Singo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huohuku akiwataka viongozi wanaokiuka katiba za vyama vyao vya michezo na kutokuwa makini kuendeleza michezo nchini, wajiondoe au waondolewe. Pia amewaasa wajumbe kuchagua viongozi wenye uwezo na moyo na kuendeleza michezo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Sehemu ya wajumbe wa mkutano huo mkuu wa uchaguzi.
Rais wa TOC, Gulam akimkabidhi zawadi ya fedha mmoja wa watumishi wa kamati hiyo kwa kutambua utendaji wao mzuri. Jumla ya watumishi watatu walituzwa.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi ambao ni viongozi wa vyama vya michezo nchini wakiwa katika mkutano huo tayari kuchagua viongozi watakao iongoza TOC kwa miaka minne hadi 2024.
Baadhi ya watumishi wa TOC
Viongozi wakuu wa TOC wakiwa na baadhi ya viongozi waalikwa kutoka serikalini.
Viongozi wakuu wa TOC wakiwa na baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇