Naibu Waziri, Ndejembi akikaribishwa na Mratibu wa Mkurabita, CPA, Dkt. Mgembe.
Naibu Waziri Ndejembi akisalimiana na watumishi wa Mkurabita.
Akiingia jengo la ofisi
Ndejembi akiwa na mwenyeji wake Mgembe ndani ya ofisi za Mkurabita zilizopo Nanenane Nzuguni.
Sehemu ya watumishi wa Mkurabita
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mkurabita, Gloria Mbilimonya akizungumza neno la utangulizi kuhusu Mkurabita na ujio wa Naibu Waziri Ndejembi.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mkurabita, Mujungu Masyenene akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mratibu wa Mkuratiba, Mgembe kutoa taarifa ya utekelezaji.
Mratibu wa Mkurabita CPA, Dkt. Seraphia Mgembe akitoa taarifa ya utekelezaji ya Mkurabita kuanzia mwaka 2004 hadi 2020.
Naibu Waziri Ndejembi akizungumza na watumishi wa Mkurabita.
Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji Ardhi na Biashara wa Mkurabita, Jane Lyimo akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri Ndejembi.
Naibu Waziri Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mkurabita.
MPANGO wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkuratiba), ni kiungo kizuri cha kuwanyanyua wanyonge nchini, sawa na mchezaji wa kimataifa Zinedine Zidane katika timu ya soka.
Kauli hiyo ameitoa Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi, alipokuwa akizungumza na watumishi wa Mkuratiba alipokwenda kujitambulisha baada ya kushika wadhifa huo.
"Mkurabita ni kiungo kizuri katika serikali kuhakikisha tunakwenda kushinda, kushinda katika kuwanyanyua wanyonge kiuchumi ili kufikia azma aliyonayo Rais John Magufuli ya kuwawezesha wananchi wanyonge waweze kuonja keki ya Taifa lao."
Ninyi ni sehemu kubwa sana ya serikali ya kuhakikisha kwamba utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, na azma ya Rais Magufuli Inafikiwa, sisi ngazi ya wizara ni kuhakikisha tunaweka mazingira mazuri kuhakikisha mnafanikiwa.
Alisema pamoja na mambo mazuri waliyofanya Mkurabita, lakini wamechelewa kwani hadi sasa halmashauri zilizofikiwa ni 52 tu kati ya halmashauri 190, hivyo inatakiwa kuongeza kasi ili zilizobaki zifikiwe.
Awali Mratibu wa Mkurabita, CPA, Dkt, Seraphia Mgembe, alisoma kwa ufupi taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha Novemba 2004 hadi Novemba 2020, kuhusu urasimishaji ardhi vijijini, mijini na urasimishaji biashara za wanyonge.
Pia, alielezea kazi ya kujenga uwezo wakulima kutumia hati miliki za rasilimali zao walizorasimisha pamoja na mafanikio kwa upande wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Alitaja baadhi ya mafanikio kuwa ni; asilimia 11 ya wamiliki wa shughuli za kiuchumi Tanzania Bara wamekopa kiasi cha sh. Trilioni 1.8 kutoka Saccos, Benki na Taasisi ndogo za fedha.
Wakulima 532 na vyama vya ushirika vitano vimetumia hatimiliki ya ardhi walizorasimisha kama dhamana na wamepata mikopo yenye thamani ya sh. bil.8.
Vilevile, Mgembe, pamoja na kuelezea mafanikio lakini aliweka wazi kuhusu baadhi ya changamoto walizonazo, ikiwemo upungufu wa fedha za kuendeshea miradi ya maendeleo, upungufu wa watumishi unaofanya utekelezaji kuwa mgumu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇