Operator Maimuna Shaban akiwa kazini katika baadhi ya mitambo ya uchapishaji katika kiwanda cha Sahl Printing kilichopo Uzunguni, Kilimani, jijini Dodoma.
Mfano wa T Shirts zilizoprintiwa kiwandani hapo.
Picha zinazofuata ni baadhi ya bidhaa zilizochapishwa kiwandani hapo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Sahl Imvestment Co.Limited, Ismail Chande akiwa katika Ofisi za Kiwanda cha Uchapishaji cha Sahl Printing. Kampuni hiyo inamiliki Sahl Real Estate.
Graphic Desigher, Joseph Katonga akiwa kazini.
Ukiingia tu katika Ofisi za Sahl Printing unapokelewa kwa bashasha na Katibu Muhtasi, Despina Sumisumi.
Muonekano wa nje ya Ofisi za Kiwanda cha Sahl Printing, Uzunguni, Kilani, jijini Dodoma.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma.
MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Sahl Imvestment Co.Limited, Ismail Chande, amepata mafanikio makubwa baada ya kuanzisha kampuni hiyo kwa mtaji wa sh. milioni 3, iliyozaa kiwanda cha uchapishaji.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii katika ofisi zake zilizopo Uzunguni Dodoma, Chande anasema licha ya huo mtaji wa sh. milioni 3 zilizotolewa sadaka kwake na watu aliowatoa majini, alioutumia kuanzisha kampuni hiyo iliyozaa pia kampuni nyingine ya Sahl Real Estate, anasema jambo lingine Kubwa lililomfanya afanikiwe ni uthubutu wake na uamuzi wake mgumu ama sivyo asingefikia hatua hiyo.
Chande ambaye ana mambo mengi na siri kubwa ya jinsi alivyoanzisha kampuni hiyo ikiwemo sadaka hiyo ya utoaji majini, ameahidi siku nyingine kuja kuelezea kwa undaji juu hayo na namna alivyohangaika kufanikisha jambo hilo pamoja na mafanikio makubwa aliyopata.
Lakini kwa leo anajikita kuelezea jinsi mwaka 2020 alivyoanzisha kiwanda cha uchapishaji cha Sahl Printing kilichopo Uzunguni, Kata ya Kilimani, jijini Dodoma, ili kuwahi fursa mbalimbali wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu na kuendelea.
Anasema ameanzisha kiwanda hicho kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata kupitia kampuni yake ya Sahl Estate aliyoianzisha mwaka 201 inayojishughulisha na ununuzi na uuzaji viwanja,nyumba, mashamba pamoja na upangishaji.
Chande ambaye alizaliwa wilayani Liwale, Mkoa wa Lindi, kuishi na kusoma shule mkoani Arusha, anasema licha ya yeye kutosomea wala kutokuwa na utalaamu wa masuala ya uchapishaji, lakini ameajiri meneja mtaalamu aliyebobea katika masuala hayo pamoja na vijana wengine 7.
Ili kuboresha biashara yake hiyo, Chande ameagiza mitambo mingine ya kisasa ya uchapishaji nje ya nchi itakayowasili nchini Januari 2020.
Ametaja baadhi ya bidhaa zinazochapishwa kwa bei poa katika kiwanda hicho kwa kuwa ni;
LARGE FORMAT;
Roll up banners, Back Drop Banners, Tear Drop Banners, 3D Letters & Acrylic, Pylons, Billboards, Vinly Stickers, Car Branding na Sign Boards.
STATIONERY MATERIALS;
Broshure, Flyers, ID Cards, Company Profile, Posters, Book Covers & Publication na Letter Heads.
PROMOTIONAL MATERIALS;
Mug (Cup printing), Pen, Gazebo, Wheel Covers, Press Banner, Moile Cases, Badges, T-shirts printing.
Ili kuendeleza sekta binafsi kwa mustakabali wa kuliletea taifa maendeleo, amewaomba baadhi ya viongozi wa Serikali kuacha kuwatisha wafanyabiashara, bali wanatakiwa wawe karibu nao kwa kuwapatia elimu, ujuzi na mikopo yenye masharti nafuu.
Lakini pia, hakusita kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Jemadari Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwawekea mazingira mazuri ya uwekezaji wazawa akiwemo yeye ambaye kwa kipindi cha uongozi wake amefanikiwa kuanzisha kampuni yenye mafanikio makubwa.
Ili nisiendelee kuharibu uhondo wa maelezo yake ya jinsi alivyofanikiwa kuanzisha kampuni na kiwanda hicho kwa kutumia sh. milioni 3 sadaka ya kutoa watu majini na uthubutu wake, basi nakusihi uendelee kumsikiliza Chande kupitia kwenye Clip hii ya Video...
RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇