LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 24, 2020

MA RC, RAS, DC, DAS NA WAKURUGENZI SASA RUHUSA KWENDA KUSHEREHEKEA KRISMASI KWAO

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amewataka watumishi wote isipokuwa wale waliozuiliwa na Waziri Mkuu, kuwa wanapaswa kwenda likizo ya sikukuu za Christmass na Mwaka Mpya kwa ajili ya kufurahia pamoja na ndugu na familia zao kwa ujumla.

Rais Dkt. Magufuli, ametoa kauli hiyo hii leo Desemba 24, 2020, wakati akiwatakia heri ya sikukuu hizo watumishi wote, mara baada ya kumuapisha Kamishna wa Maadili aliyemteua hapo jana, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi, Ikulu ya Chamwino Dodoma.

“Wale mtakaoweza kusafiri kuwaona ndugu zenu ni ruksa siku mbili tatu au tano, kwenda kumuona mama yako si vibaya, hakuna dhambi kufika nyumbani, wengine mtaenda kufanya matambiko, isipokuwa wale waliouzuiliwa na Waziri Mkuu, nafikiri ni wakurugenzi na watu wengine wanaotakiwa kuwajibika ili shule zitakapofunguliwa kuwepo na madarasa, lakini wengine Ma DAS, DC, RC ni lazima mjipange ili ofisi msiziache wazi” JPM

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages