Msanii wa Muziki wa Injili Boniface Mwaitege akitoa ombi kwa serikali kuwasaidia wasanii wa Muziki wa Injili wanao dhulumiwa haki zao na moja ya kampuni (jina limehifadhiwa) ya usambazaji wa nyimbo za injili njia ya mtandao, leo Desemba 05, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika kikao cha kujadili mikakati ya kuendeleza sekta ya sanaa kwa wanamuziki wa injili kufuatia tamko la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuendeleza Sanaa wakati alipokuwa akifungua Bunge
Msanii wa Muziki wa Injili
Christina Shusho akitoa ombi kwa serikali la kuandaliwa kwa Tuzo za Muziki wa
Injili nchini ili kutoa hamasa kwa wasanii hao, leo Desemba 05, 2020 Jijini Dar
es Salaam, katika kikao cha kujadili mikakati ya kuendeleza sekta ya sanaa kwa
wanamuziki wa injili kufuatia tamko la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuendeleza Sanaa wakati alipokuwa
akifungua Bunge.
Msanii wa Muziki wa Injili Emmanuel Mgaya akitoa ombi kwa serikali la kuangalia suala la gharama za kusajili Youtube Channel kuwa ni kubwa sana kwa kundi la wasanii, kwani wao hutumia akaunti hizo kutafuta masoko ya kazi zao na siyo kuhabarisha umma, leo Desemba 05, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika kikao na Wanamuziki wa Injili kujadili mikakati ya kuendeleza tasnia sekta ya sanaa kufuatia tamko la Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akifungua Bunge.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇