LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 17, 2020

BILIONEA SUBASH PATEL AFANYIWA MAZIKO YA MWILI WAKE KUCHOMWA MOTO, KATIKA MAKABURI YA WAHINDU, JIJINI DAR ES SALAAM, LEO


CCM Blog, Dar es Salaam

Maziko ya aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni za Motisun Group  ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) Subash Patel yamefanyika kwa mwili wake kuchomwa moto leo katika makaburi ya Wahindu yaliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.


Katika maziko hayo Msemaji wa Kampuni za Motisun Group,  Aboubakari Mlawa amesema Subhash Patel aliyefariki usiku wa kuamkia juzi akiwa nyumbani kwake, Kisutu Jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akiendelea na matibabu, alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na ameacha mke mmoja na Watoto wawili.

 

Mfanyabiashara huyo maarufu nchini alikuwa akimiliki kampuni zinazotengeneza bidhaa za plastiki, saruji, mabati, nondo, nyaya za umeme, vinywaji, rangi na pia alimiliki hoteli za White Sands na Sea Cliff, Pearlsun Hotel & Resorts.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages