LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 3, 2020

UCHAGUZI MKUU WA MWAKA HUU UMEACHA SOMO LA KIHISTORIA KWA WANASIASA WA CCM NA WA UPINZANI

*Iliyoyapata CHADEMA ndiyo matokeo ya kuteua mgombea mwenye mdomo usio na breki

Na Kalamu ya Mwigamba

UCHAGUZI Mkuu wa mwaka 2020 umefanyika wiki iliyopita, Jumatano Oktoba 28, 2020. Lakini kama tulivyowahi kutabiri ulikuwa ni uchaguzi wa kihistoria ulioacha masomo ya kihistoria kwa wanasiasa wote, wa chama tawala na upinzani. Kwa chama tawala ni dhahiri wameelewa kwamba watanzania hawajawahi kuichukia CCM.

Watanzania wana historia na CCM kama chama kilichozaliwa na TANU na ASP, vyama vilivyoleta uhuru wa Tanganyika na Zanzibar. CCM iliasisiwa na waasisi wa taifa hili ambao wana heshima kubwa katika taifa hili. Muasisi namba moja wa CCM ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, binadamu mwenye heshima kubwa ndani ya nchi hii.

Kilichokuwa kinawaudhi watanzania mpaka kutoa viti vingi vya ubunge na udiwani kwenye vyama vya upinzani ni kitendo cha viongozi wa CCM waliokuwepo kuacha misingi ya chama na ya taifa hili na kugeukia vitendo viovu vya ufisadi, ufujaji mali ya umma, kukumbatia matajiri, kuporomosha nidhamu ya utumishi wa umma, nk.

Kitendo cha CCM kujitathmini na 2015 wakapitisha viongozi wasio na tuhuma ya rushwa, wachapakazi, wazalendo na wapenda nchi, kilianza kuwarudishia matumaini watanzania. Ndiyo maana pamoja na ushindani uliokuwepo kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, bado walikipa chama hicho nafasi ya kuendelea kushika dola.

Na kweli kama ilivyotarajiwa, viongozi hao wakiongozwa na Jemedari John Pombe Magufuli wakafanya maajabu. Wameirejesha nchi hii kwenye misingi ya waasisi wake na kupiga hatua kubwa za maendeleo katika muda mfupi huku wakikaribia kutowesha rushwa na ufisadi. Sasa watanzania wanaamini asilimia 100 kwamba CCM imerejea kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi, watu wanyonge. Ushindi kiliopata CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni ushahidi wa imani hiyo ya watanzania.

Somo kubwa walilojifunza viongozi wa CCM waliopo na watakaokuja, ni kwamba chama hakitakiwi kurudi nyuma. Yaani hata itakapotokea Rais Magufuli akaondoka madarakani, Mwenyekiti mpya wa CCM aendeleze moto ule ule wa Magufuli ili nchi iendelee kupaa kimaendeleo. Wakifanya hivyo, wanaweza kuendelea kuaminiwa na watanzania kuendelea kuwa chama tawala.

Kwa upinzani, kama hawatatuelewa sasa basi hawatatuelewa milele! Kama kuna wanasiasa tumewaasa, tumewashauri, tumewakemea, tumewaonya, tumewasaidia, tumewaelekeza, basi ni wanasiasa wa upinzani. Bahati mbaya mashauri yetu yote yamekuwa kama mbegu zinazoangukia juu ya miamba na hatimaye kupeperushwa na upepo na kushindwa kuota na kuzaa mazao.

Ndiyo maana hata sasa wanaendelea kufanya makosa. Tamko walilolitoa haraka haraka baada tu ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa, lilikuwa ni tamko lililotolewa kwa harara, wakiwa na hasira, na kwa ujumla limekuwa ni kosa lingine la kiufundi (technical mistake). Walitakiwa kutulia, kujishusha na kutoa tamko la kuonyesha kweli kwamba ni wazalendo kwa taifa lao.

Kwa mfano wangeweza kuwaambia watanzania hayo wanayodhani yalikuwa ni mapungufu kwenye uchaguzi na kusema hata kama hawajaridhika na matokeo lakini Tanzania ni kubwa kuliko wao. Kwa faida ya taifa letu na watu wake, wameamua kuyakubali matokeo, watafanya utafiti usioegemea upande wowote wakiwauliza watanzania kwa nini wamewanyima kura na hatimaye wajipange upya kwa uchaguzi wa 2025.

Wawaombe wanachama wao na watanzania kwa jumla wawaunge mkono kwa hilo kwa kutofanya vurugu yoyote na viongozi wa dini wawaunge mkono. Wawaahidi wanachama wao na watanzania kwamba chochote watakachowaeleza kwamba kilikuwa ni sababu ya kuwanyima kura wao na vyama vyao, watakifanyia kazi na kuandaa mikakati mipya kuelekea uchaguzi mkuu ujao. 

Wangefanya hivyo, leo hii kila kona tungekuwa tunasikia kauli za viongozi wa dini, viongozi wastaafu, wachambuzi wa masuala ya kisiasa na wananchi wote wakiwasifu kwa ukomavu wa kisiasa.

Wangefanya hivyo na kutekeleza yote watakayoambiwa na watanzania kwa nini uchaguzi ujao wasiungwe mkono na wapigakura? Akina Freeman Mbowe wanajua kwamba hiki ninachowashauri si kigeni, CCM walikifanya baada ya uchaguzi wa mwaka 2010. Baada ya kupoteza majimbo mengi na kura za mgombea urais zikapungua kutoka 80% ya mwaka 2005 mpaka 61% kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, waliunda kamati iliyoongozwa na Wilson Mkama.

Ni kamati ya Mkama iliyogundua kwamba watanzania waliichukia CCM kwa sababu ya tuhuma za ufisadi. Ndipo wakaja na mkakati wa ‘kujivua gamba’ wakiwataka wana CCM waliokuwa wanatuhumiwa kwa ufisadi kujiuzulu nyadhifa zao. Kwenye uchaguzi wa 2015 wakawakata watuhumiwa wote wa ufisadi na matunda yake yameonekana kwenye uchaguzi wa mwaka huu.

CHADEMA na ACT badala yake wamekimbilia kutangaza maandamano ambayo wanajua kabisa kwamba hayatawapa matunda yoyote. Kwanza siwaoni waandamanaji watakaoshinda barabarani kila siku bila kukoma. Mbowe hataki kukubali kwamba chama kimepoteza mvuto kwa kupoteza wanachama wengi ambao wengi wao wameondoka au kufukuzwa katika jitihada za Mbowe kuhakikisha anaendelea kushikilia kiti cha uenyekiti.

Lakini pia vijana waliokuwa wanapambania chama kama makamanda wakiwemo red brigade wote wamekata tamaa na ama kukimbia au kubaki kwenye chama kama wanachama mfu. Wameshuhudia chama kikiongeza viti vya ubunge na ruzuku lakini hawaoni hizo pesa zinaishia wapi wao kila leo wanaambiwa ‘wakomae’. Kwa ujumla vijana wamechoka na siasa za CHADEMA na siwaoni wa kuandamana mfululizo eti wakipigania Mbowe na akina Lema warudi bungeni.

Lakini pili, hivi Mbowe na Zitto wanaposema uchaguzi urudiwe na usimamiwe na tume nyingine wanayoiita huru, hiyo tume wanayoitaka si ndiyo iliingizwa kwenye katiba mpya iliyokuwa inapendekezwa na wao wakaikataa katiba hiyo na kususia mchakato mzima? Sasa leo wanataka nini? Hivi wakiandamana mfululizo lakini Rais Magufuli anaendelea na kuunda serikali na kufanya kazi wanayoitaka watanzania, hayo maandamano yao yataendelea mpaka lini?

CHADEMA walidanganywa na mafanikio ya mwaka 2015, lakini kwa maoni yangu mafanikio yale hayakuwa ya CHADEMA bali yalikuwa ni ushahidi wa nguvu aliyokuwa nayo Lowassa ndani ya CCM. Mafanikio halisi ya CHADEMA ni yale yaliyopatikana mwaka 2010 chini ya kinara wake Dkt. Willibrod Slaa. Hayo ndiyo walitakiwa kuyaendeleza mwaka 2020.

Kilichotokea mwaka huu ni kwamba mafanikio ya Slaa yaliondoka naye mwaka 2015, na yale ya Lowassa yalirudi naye aliporejea CCM. Haya waliyoyapata hivi sasa ndiyo mafanikio yao halisi ya sasa, ndiyo matokeo ya kuteua mgombea msema hovyo ambaye mdomo wake hauna breki. Freeman Mbowe, Benson Kigaila, John Mnyika, na wengineo wote, wanajua kwamba wamemkatalia Lissu mara mbili (2009 na 2014) kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA kwa sababu hizo hizo za kukosa breki mdomoni.

Walitoa hoja kwamba hana staha, hachagui maneno ya kuongea anaropoka tu kama kichaa, atakwaza wanachama wapya kujiunga na chama hicho. Lakini ni hao hao waliotegemea watanzania wampe Lissu kura kama zile walizompa Slaa au walizompa Lowassa, kama siyo ujinga ni nini? Kama hawataki kupoteza hata hiyo imani kidogo waliyobaki nayo kwa watanzania, waachane na mpango wa maandamano waonyeshe kwamba wamekomaa kisiasa.

Na kosa la pili ambalo naliona wanaenda kulifanya ni kwenye uteuzi wa wabunge wa viti maalum. Najua kabisa kwamba utakuta wameorodhesha wabunge wale wale maswahiba wa Mbowe akina Halima Mdee, Esther Bulaya, Esther Matiko, nk. Wale wale waliotuhumiwa na Sabreena Sungura kwamba umaarufu wao ndani ya CHADEMA unatokana na kuvuta vitu visivyokuwa vya kawaida kisha wakaenda kutukana viongozi wa serikali bungeni.

Hawa akina Mdee na Bulaya wana mchango kwenye anguko la CHADEMA kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Walishirikiana na akina Gobless Lema, Peter Msigwa na wengine kugeuza bunge kuwa uwanja wa fujo badala ya kuwakilisha wananchi waliowachagua. Walikuwa hawatoi hoja za zinazojali maslahi ya watanzania bali walikuwa wanawakilisha matakwa yao na ya chama chao. Watanzania walikidharau chama kwa ajili ya hawa.

Lakini watawaacha wanawake wengine wa CHADEMA wastaarabu walioomba viti maalum na kuwarudisha hawa akina Mdee ambao wamekaa bungeni kwa miaka kumi na zaidi. Hawako tayari kujaribu vipaji vingine ili waone kama hao wapya wataweza kukivusha chama chao kwa kutoa hoja zenye mashiko bungeni.

Na bado wanawake wa CHADEMA walioomba ubunge wa viti maalum watakubali uonevu huu na kunyamaza kimya. Wako tayari kuona viongozi wao wa chama wanapeleka watu wao bungeni kupitia viti maalum kila uchaguzi na wao wanafyata tu mkia na kunyamaza bila kupaza sauti zao. Wataendelea kuonewa mpaka lini? Wengine wanafanyiwa vitendo vibaya kama walivyodai akina Suzan Massele na Joyce Sokombi.

Wanafanyiwa vitendo vya hovyo na ubunge wananyimwa halafu wananyamaza na kugugumia kimya kimya. Ukimya wao unawafanya viongozi wao kuendelea na matendo hayo kwa wengine. Lakini hawa jamaa wakirudia mchezo huo mwaka huu halafu wale waliooachwa wakajitokeza kupinga hadharani, watakomesha tabia hii.

Yote kwa yote sisi wengine kazi yetu kuwaambia tu ukweli CHADEMA na kuwaacha wafanye uamuzi wenyewe. wakiendelea kushupaza shingo na kutegemea watachaguliwa tu na watanzania, tuonane 2025!

Na Kalam ya Mwigamba

UCHAGUZI Mkuu wa mwaka 2020 umefanyika wiki iliyopita Jumatano Oktoba 28, 2020. Lakini kama tulivyowahi kutabiri ulikuwa ni uchaguzi wa kihistoria ulioacha masomo ya kihistoria kwa wanasiasa wote, wa chama tawala na upinzani. Kwa chama tawala ni dhahiri wameelewa kwamba watanzania hawajawahi kuichukia CCM.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages