LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 10, 2020

RAIS WA COMORO AONDOKA NCHINI LEO, AISIFU TANZANIA KWA KUFANYA UCHAGUZI KWA AMANI NA UTULIVU

Rais wa Visiwa  vya Comoro, Azali Assouman na mkewe wakipunga mikono kuaga baada ya kuingia kwenye Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, tayari kwa ajili ya kuondoka kurudi nyumbani, leo. Rais huyo alikuwa hapa nchini kushuhudia hafla ya Uapisho wa Rais Dk. John Magufuli iliyofanyika Novemba 5, 2020, Jijini Dodoma na Baadaye alitembelea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro


Habari Kamili👇

Dar es Salaam, Tanzania

Rais wa Visiwa vya Comoro Azali Assouman, aliyekuwa hapa nchini kushuhudia uapisho wa Rais Dk. John Magufuli uliofanyika jijini Dodoma siku tano zilizopita, ameondoka leo kurudi nyumbani huku akiipongeza Serikali ya Tanzania kwa kufanya uchaguzi huru, amani na haki.


Assouman ametoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kabla ya kuondoka na kuongeza kuwa imethihirika kuwa Tanzania ni nchi ya Amani na utulivu wa kisiasa kwani wakati wote wa tukio la kuapishwa kwa Dk. Magufuli aliona mambo ambayo yanapaswa kuigwa na mataifa mengine hususan kwenye nyakati za uchaguzi.


"Kwa kweli tangu nimefika hapa Tanzania nimeona mambo mazuri na ambayo tunapaswa kuyaiga sisi viongozi wa mataifa mengine," Amesema Rais Assouman


Mbali na kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo ya uchaguzi, pia Rais Assouman ameliahidi ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika Nyanja za mbalimbali ikiwemo diplomasia ya uchumi, biashara, uwekezaji na utalii.


“Najisikia niko nyumbani kwa sababu uhusiano wetu umeimarishwa zaidi, mahusiano yetu yamekuwa katika masuala ya kijamii, utamaduni, biashara na mambo mengine mengi” Amebainisha Rais Assouman.


Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Sylvester Mabumba amesema kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Comoro katika kuhakikisha kuwa sera ya uchumi wa nchi zote mbili unakua zaidi.


"Sisi tuatendelea kushirikiana vyema na Comoro kibiashara ili kukuza sera ya 2025 tunaifikia ipasavyo kwa kuhakikisha kuwa uchumi wetu unafikia kiwango cha juu sana, naamini kuwa tunapokuwa na masoko ya uhakika Viswa vya Comoro uchumi wetu utakuwa zaidi," Amesema Balozi Mabumba.


Kwa Upande wake Balozi wa Visiwa Vya Comoro nchini Tanzania Dk. Ahmada El Badaoui Mohammed amesema kuwa kuna fursa nyingi za kiuchumi ambazo Comoro na Tanzania zinaweza kushirikiana.


Rais Assouman aliwasili nchini Novemba 4 kwa ajili ya kuhudhuria hafla ya uapisho wa Rais Dk. John Magufuli uliofanyika Novemba 5 Jijini Dodoma ambapo baada ya shughuli hiyo alipata fursa ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ambapo na kujiona vivutio mbalimbali vya utalii nchini.


Serikali ya Tanzania na Visiwa Comoro zimekuwa zikishirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo, elimu, afya, biashara na uwekezaji.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages