Rais Mteule Dkt. John Pombe
Magufuli akipokea Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais kutoka kwa Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage, katika Hafla ya kumkabidhi cheti hicho kufuatia kushinda Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini, Jumatano, Oktoba 28, 2020. Hafla hiyo imefanyika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) eneo la Njedengwa jijini Dodoma, leo, Novemba Mosi, 2020.
Dk Magufuli akionesha cheti hicho
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Cheti cha Ushindi wa Kiti cha
Makamu wa Rais kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji
Mstaafu Semistocles Kaijage.
Rais Mteule Dk. Magufuli akitoa neno la shukran.
Dkt.
John Pombe Magufuli akimpongeza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
mara baada ya kukabidhiwa Cheti cha Ushindi
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na Waliogombea Urais kupitia vyama
Mbalimbali vya Upinzani nchini wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa katika hafla fupi
ya kukabidhi Cheti cha Ushindi.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na
Kiongozi wa Jopo la Waangalizi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Katika Uchaguzi
Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020 Rais Mstaafu wa Burundi Silvestre
Ntibantunganya mara baada ya kukabidhiwa Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais
kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu
Semistocles Kaijage leo tarehe 01 Novemba 2020.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇