LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 2, 2020

DK. HUSSEIN ALI HASSAN MWINYI AAPISHWA LEO KUWA RAIS WA ZANZIBAR

Dk.Hussein Ali Haasan Mwinyi  akipa kuwa Rais wa awamu ya nane ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar alipoapishwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othuman Makungu katika sherehe za kumuapisha zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar, leo.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akimuapisha Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakati wa  sherehe za kiumuapisha zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar, leo. Aliyeketi akishuhuia ni Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein. Matukio mengine yahanyohusu sherehe hiyo tutaweka baadaye. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akikagua gwaride maalum la vikosi vya ulinzi mara baada ya kuapishwa rasmin  kufuatia ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu Uliopita, kushika wadhifa wa Urais awamu ya 8 ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hafla iliyofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studium Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akikagua gwaride maalum la vikosi vya ulinzi mara baada ya kuapishwa rasmin  kufuatia ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu Uliopita, kushika wadhifa wa Urais awamu ya 8 ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hafla iliyofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studium Jijini
 Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akipongezwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mzee Ali Hassan Mwinyi  Mwinyi baada ya kuapishwa rasmin kushika wadhifa huo  awamu ya nane ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hafla ilifanyika leo katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akipongezwa na Mkewe Mama Marium Mwinyi mara baada ya kuapishwa rasmin    kushika wadhifa huo  awamu ya nane ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hafla ilifanyika leo katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akipongezwa na Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha  mara baada ya kuapishwa rasmi leo  kushika wadhifa huo  kwa awamu ya 8 ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hafla iliyofanyika   katika Uwanja wa Amaan Studium Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akipongezwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume  baada ya kuapishwa rasmi leo  kushika wadhifa huo  kwa awamu ya nane ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hafla iliyofanyika   katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akipongezwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kuapishwa rasmi leo  kushika wadhifa huo  kwa awamu ya nane ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hafla iliyofanyika   katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akipongezwa Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, baada ya kuapishwa rasmi leo  kushika wadhifa huo  kwa awamu ya nane ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hafla iliyofanyika   katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa ameketi huku akitafakari wakati alipokuwa akisubiri kuapishwa. Kuhsoto ni Maakamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya Viongozi wakiwa kwenye sherehe hiyo. Kushoto, mstaari wa mbele ni Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Zanzibar Mzee Ali Hassan Mwinyi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliyemaliza muda wake, Balozi Ali Seif Idi.
Baadhi ya waliohudhuria sherehe hiyo.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe hiyo. (Picha zote na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages