LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 4, 2020

DIWANI MTEULE WA KIVUKONI SHARIK CHOUGHLE ATEMBELEA SOKO LA SAMAKI FERI KUJUA KERO ZILIZOPO KATIKA SOKO HILO

Diwani mteule wa Kata ya Kivukoni jijini Dar es Salaam, Sharik Choughle jana alianza kazi kwa kutembelea soko Kuu la Samaki la Feri ili kujua kero zinazowakabili wafanyabiashara mbalimbali na shughuli nyingine katika soko hilo na pia kuwashukuru kwa kumchagua yeye, Mbule wa Ilala na Dk. John Magufuli kuendelea kuwa Rais wa Tanzania. Pichani, Diwani Sharik akitazama samaki aina ya Sangara waliofikishwa katika soko hilo kutoka Mwanza na kutaka kujua kama samaki hao wanafika wakiwa bado wana ubora na eneo wanakohifadhiwa kabla ya kuuzwa.
Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle akitazama paa la jengo katika eneo la wauza viungo katika soko la Feri baada ya wafanyabiashara katika eneo hilo kulalamikia kuwa linavunja nyakati za mvua.
Diwani huyo mteule akizungumza na wafanyabiashara wa eneo la viungo katika soko hilo baada ya kusikiliza kero zao
Diwani huyo Mteule akisalimiana na mmoja wa Vijana wapakuaji mizigo kutoka katika magari katika soko hilo
Diwani Mteule wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle akisalimiana na Mzee mfanyabiashara ya samaki katika soko hilo
Diwani Mteule wa Kata ya Kivukoni Shariki akisalimiana na Mfanyabiashara katika soko hilo.

Sharik akikagua Ujenzi wa Kontena la kuhifadhia samaki katika Soko hilo la Feri đź‘‡





Fundi akipaua Kontena hilo.

Sharik akisikiliza kero kwenye eneo la kuhifadhia samaki na bidhaa nyingine kutoka baharini👇

Shariki akizungumza na maafisa katika soko hilo pamoja na viongozi wa Kata aliofuatana nao kwenye ziara hiyo.

Akikagua nguzo ya jengo la la wafanyabishara eneo la kuhifadhi na kuuza samaki.👇




👆Shariki akitoa maelekezo baada ya kukagua nguzo hiyo. Kisha akaendelea na ziara yake👇


"Miwa bei gani?" Shariki akimuliza mfanyabiashara ya miwa katika soko hilo la Feri👇


Kisha Diwani huyo mteule akanunua miwa na kumwagiza muuzaji wa miwa hiyo kuzingatia usafi wa mazingira kwa kutotupa hovyo maganda baada ya miwa kumenywa.

Mama muuza supu akiwa na mteja wake katika soko hilo la Feri, wakati wa ziara hiyo ya Diwani mteule wa Kata ya Kivukoni Shariki Choughle👇



Diwani Mteule wa Kata ya Kivukoni Shariki Choghule akisalimiana na Afisa wa Umoja wa Wavuvi Wadogo wadogo wa Kivukoni, Amina Hussein, alipofika kwenye Ofisi ya Umoja huo.
Mmoja wa viongozi wa Umoja wa Wavuvi Wadogo Wadogo wa Kivukoni Amran Yahya akimuonyesha Sharik, majitaka yanavtotiririka na kuharibu mazingira. Kwa mujibu wa kiongozi huyo sehemu kubwa ya majitaka hayo ni haja ndogo ambapo ameomba choo kiboreshwe ili majitaka hayo yasiwe yanatiririka.
"Hallo, Hallo", Sharik akapiga simu papo hapo wa Mtendaji wa Kata hiyo ya Kivukoni kumuomba ashughulikie haraka kero hiyo.

Shariki akiwa na Mamalishe katika soko hilo👇



Sharik akizungumza na Viongozi wa Umoja wa Wavuvi Wadogo wadogo alipofika ofisini kwao akiwa katika ziara hiyo.

Diwani Sharik akitazama samaki aina ya Sangara waliofikishwa katika soko hilo kutoka Mwanza na kutaka kujua kama samaki hao wanafika wakiwa bado wana ubora na eneo wanakohifadhiwa kabla ya kuuzwa. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO- CCM Blog
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages