LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 15, 2020

ASKOFU GWAJIMA ALIVYOWAVUNJA MBAVU RAIS MAGUFULI, SPIKA NDUGAI NA WABUNGE

Mbunge mpya wa Jimbo la Kawe, Dar es Salaam, Askofu Josephat Gwajima ‘aliwavunja mbavu’ Rais  Dk. John Magufuli, Spika Job Ndugai, viongozi wengine wakuu, wabunge na wageni waalikwa  alipotoa neo la utani kwa watani wao Wasukuma, Wagogo kuwa enzi hizo Baba wa Taifa, Julius Nyerere aliwaambia Wagogo wapanue mashamba yao ili yawe makubwa wapate mazao mengi , lakini wao hawakumuelewa, badala ya kupanua mashamba wao wakapanua masikio.

Hiyo ilionekana kama ni majibu ya utani aliousema Spika Ndugai  bungeni mwishoni mwa wiki kuwatania watani wao Wasukuma kuwa wameingia jijini Dodoma, hivyo kwa’ ushamba wao’ wawe wanangalia vizuri barabrani wasije wakagongwa na magari. Gwajima ni msukuma na Ndugai ni Mgogo hivyo utani kwao ni kitu cha kawaida.Tukio hilo la aina yake la kuchekesha lilitokea wakati SpikaNdugai alipompatia fursa Askofu Gwajima kutoa neo la shukrani kwa niaba ya wabunge baada ya Rais Magufuli kulifungua rasmi Bunge la 12 Novemba 13, 2020.


Askofu Gwajima akitoa neno la shukrani baada Rais Magufuli kufungua rasmi Bunge la 12 jijini Dodoma Novemba 13, 2020 ambapo pia aliwatania watani wao Wagogo.


Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Mrema pamoja na wageni waalikwa wengine wakicheka kutokana na utani wa Askofu Gwajima.


Imeandaliwa na Richard Mwaikenda

Mhariri Blog ya Taifa ya CCM

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages