Na Mwandishi Wetu, MUSOMA
Mabingwa wa kihistoria Tanzania bara timu ya Yanga SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Biashara United katika Uwanja wa Karume, mjini Musoma mkoani Mara.
Bao pekee la Yanga SC limefungwa na mshambuliaji wake Mghana, Michael Sarpong dakika ya 68 akimalizia krosi ya Ditram Nchimbi kutoka upande wa kulia.
Huu umekuwa ushindi wa saba mfululizo katika mchezo wa nane wa msimu, unaifanya Yanga SC inayofundishwa na kocha Mrundi, Cedric Kaze ifikishe pointi 22, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa wastani wa mabao na Azam FC ambayo imecheza mechi moja zaidi.
Yanga bado wapo kanda ya ziwa hii ni mechi ya pili kushinda baada ya kuitandika KMC mabao 2-1 na itateremka tena uwanjani Novemba 3,2020 kuwakabiri wenyeji Gwambina FC
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇