LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 10, 2020

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA - TANESCO YAWAFIKIA WATEJA WENGI MITAANI

Katika kuadhimisha wiki ya Huduma kwa Wateja,  Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  kupitia watoa huduma wake toka maeneo mbalimbali wamewafikia Wateja mitaani na kutoa elimu na huduma mbalimbali zihusuzo huduma na bidhaa za TANESCO.

 

Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano TANESCO, Bi. Johari Kachwamba wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja leo Ijumaa Oktoba  09, 2020 kwenye viwanja vya Biafra Kionondoni jijini Dar es Salaam.


”Tangu Oktoba 5, tumekuwa tukitoa huduma mbalimbali kwa wateja wetu kote nchini, tumetoka ofisini na kuwafuata wateja mitaani waliko na hadi leo hii tunaadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja katika  Mkoa wetu wa Kinondoni Kaskazini ambapo pekee tumewahudumia wateja wengi waliotutembelea katika viwanja vya Biafra Jijini Dar es Salaama” alisema Bi. Kachwamba. 


Aliongeza kuwa, Wiki ya huduma kwa wateja imekuwa ni fursa nzuri na adhimu kwa TANESCO na wateja wa Shirika kukutana. 


Alisema, miongoni mwa huduma zilizotolewa na wafanyakazi wa TANESCO kwa wateja ni pamoja na elimu ya matumizi bora na salama ya umeme, kuwasikiliza wateja, wateja wameweza kujaza fomu za maombi mapya ya kuunganishiwa umeme, na pia wameelimishwa kuhusu aina mbalimbali za mita za umeme.


Akimuwakilisha Meneja wa Kinondoni Kaskazini, Mhandisi Godlove Mathayo, wateja wengi wamekuwa wakifanya wayaring kwenye nyumba zao bila kutumia Wakandarasi waliosajiliwa hivyo wateja wameelimishwa kutambua na kutumia Wakandarasi waliosajiliwa kwa usalama wao na mali zao kuepusha hitilafu za umeme za mara kwa mara.


“Niwashauri wateja wetu wanapotaka kufanya wayaring wawatumie mafundi walioidhinishwa na EWURA kwani hao wana ujuzi wa kutosha wa kufanya kazi hiyo" alisema Mhandisi Mathayo.


Mhandisi Mathayo alifafanua kuwa, mteja anapotaka kufikishiwa umeme halazimiki kulipa gharama yoyote ya ukaguzi wa eneo (survey) kwani huduma hiyo inatolewa bure na TANESCO.

Mteja wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO (kulia) akitoa maelezo yake huku wahudumu wa TANESCO wakimsikiliza kwa makini wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya Huduma kwa Wateja kwenye viwanja vya Biafra , jijini Daar es Salaam Oktoba 9, 2020.

.


Wananchi wakiwa kwenye banda la TANESCO viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam ili kupata elimu ya matumizi sahihi na Salama ya umeme wakati wa kilele cha wiki ya Huduma kwa Wateja Oktoba 9, 2020.
Mfanyakazi wa TANESCO akitoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya mita wakati wa kilele cha wiki ya Huduma kwa Wateja kwenye viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es Salaam Ijumaa Oktoba 9, 2020.

Afisa Uhusiano Tanesco Wilaya ya Tegeta, Khadija Faru, akitoa elimu ya matumizi Bora na Salama ya umeme wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kaskazini, Eng. Godlove Mathayo, akizungumza kwenye kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam Oktoba 9, 2020.

 Meneja Uhusiano,TANESCO  Makao Makuu, Bi. Johary Kachwamba, akizungumza kwenye kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam Oktoba 9, 2020.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages