LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 12, 2020

WANAWAKE TUNA JAMBO LETU OKTOBA 28, NI KUWAPIGIA KURA WAGOMBEA WA CCM-OKASH

MGOMBEA Ubunge Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Halima Okash  akinadi sera nzuri za CCM pamoja na kuwaombea kura wagombea wa chama hicho katika mkutano wa kampeni katika Kata ya Ikombolinga Jimbo la Mvumi, Dodoma.
Sehemu ya wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni katika Kata ya Ikombolinga, Mvumi.
Okash akiomba kura kwa unyenyekevu kwa ajili ya wagombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28.
 

Na Mwandishi wetu, Mvumi.

MGOMBEA Ubunge Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Halima Okash amewakumbusha wanawake kuwa Oktoba 28, wana jambo lao muhimu, nalo si lingine, bali kuwapigia kura wagombea wote wa CCM.

Amewasihi siku hiyo kuamka asubuhi na mapema kwenda kumpigia kura Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli, Mgombea Ubunge Jimbo la Mvumi, Livingstone Lusinde na wagombea udiwani wa CCM.

Okash aliyasema hayo akiwa katika kikao cha ndani cha kampeni za CCM katika Kata ya Maka'ngwa Jimbo la Mvumi ambapo alikutana na viongozi na wanawake. 

"Wanawake tuna jambo letu Oktoba 28, ni kuhakikisha kwanza tunamrudisha mbunge wetu, Lusinde lakini pia tunampigia kura za kishindo Mgombea Urais wa CCM, Dk.Magufuli na madiwani wetu wote wa CCM," alisisitiza Okash huku akipigiwa makofi. 

"Si kwamba tutapiga kura za huruma kwa wagombea hao,bali tutapiga kwa Dk Magufuli kwa sababu ameleta maendeleo yanayoonekana hasa katika Mkoa wetu wa Dodoma na Nchi kwa ujumla katika seka za afya, elimu, miundombinu nishati ambavyo wanufaika wakubwa ni akina mama na watoto," alisema Okash.

Alitaja baadhi ya mambo ambayo Mkoa wa Dodoma umenufaika wakati wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Dk. Magufuli kuwa ni; Dodoma kutangazwa kuwa Jiji, kuhamishia makao makuu ya nchi, Rais kuhamia Ikulu ya Chamwino, Ujenzi wa Stendi ya Kisasa kubwa kuliko zote nchini na Afrika Mashariki yenye uwezo wa kuegesha mabasi 600 kwa wakati mmoja.

Miradi mingini ni, Soko la Kisasa la Job Ndugai, Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR, kuanza kwa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato na kuanza ujenzi wa barabara za pete (Ringroads) kulizunguka jiji la Dodoma na hivi karibuni JPM ametangaza kujenga Uwanja Mkubwa wa Kisasa wa michezo.

Pia, Okash aliwaasa wanawake kuacha tabia ya kuwapigia kura watu waoenda kufanya majaribio ya uongozi, bali wampatie kura Dk. Magufuli na wagombea wengine wa CCM chama chenye watu wenye uzoefu wa kuongoza nchi.

Akiwa katika kikao cha ndani katika Kata ya Ikombolinga, Jimbo la Mvumi, Okosh aliwaombea kura Dk Magufuli, Lusinde na Mgombea Udiwani wa kata hiyo, Mtemi Matonya na kuwasihi wanawake kuwa mabalozi wema kuzisaka kura za wagombea hao.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages