LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 23, 2020

Video:NI KWELI MAGAIDI 300 WALIVAMIA MTWARA, BAADHI WANASWA=IGP SIRRO

 

“Ni kweli Wiki iliyopita, Magaidi wapatao 300 walitoka Msumbiji walivamia kituo chetu pale Kijiji chetu cha Kitaya (Mtwara), walifanya uhalifu mbalimbali na walifanya mauaji, tumefuatilia na baadhi ya Watuhumiwa kadhaa siwezi kuwataja wamekamatwa kuhusika na hayo matukio ambao wengine ni wa kwetu hapa walishirikiana na wengine kutoka nje”– IGP Sirro

“Kwakuwa tunaendelea na huo mtandao siwezi kusema sana lakini niwahakikishie Watanzania kwamba siku zote huwa nasema damu ya Mtanzania haipotei bure, waliofanya mauaji wengine wamerudi Msumbiji waliobaki tumewakamata tunaendelea kuwahoji kuhusu mtandao mzima”– SIRRO

“Watanzania waelewe huu ni mtandao ambao ulianzia Rufiji, Kibiti wengine tulipambana nao wakaona wameshindwa wakakimbilia Msumbiji, kule wameungana na wenzao wanajaribu kurudi nyumbani, tumejipanga kuwa wakirudi tutawashughulikia na hata wakibaki huko tutashirikiana na wenzetu kuhakikisha hawatokuwa salama”– SIRRO

 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages