LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 10, 2020

Video & Picha: GOMBO MGOMBEA UDIWANI MWENYE MISIMAMO YA KIMAENDELEO, ATANGAZA NEEMA IPAGALA DODOMA MJINI



Mgombea Udiwani wa Kata ya Ipagala, Dodoma Mjini, Gombo Kamuli Dotto akiwa na furaha wakati wa kampeni zake zilizofanyika katika Mtaa wa Mlimwa Kusini ambapo alielezea mafanikio yaliyopatikana wakati wa kipindi chake cha miaka mitano iliyopita na kutangaza mambo lukuki ya kimaendeleo anayotarajia kuyafanya endapo atapigiwa kura na kushinda Oktoba 28, 2020.


Mwenyekiti wa CCM Tawi Mlimwa Kusini,Mohamed Keba akimwaga sera za CCM alipokuwa akifungua mkutano wa kampeni.                        
Wananchi wakishangilia wakati Mgombea Udiwani wa Kata ya Ipagala, Gombo akielezea mafanikio aliyofanya katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake.


Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma 2015-2020 ambaye aliwania tena nafasi hiyo lakini kura hazikutosha, akiwaombea kura wagombea wa CCM, Dk. John Magufuli, Mgombea Ubunge Dodoma Mjini, Anthony Mavunde na Mgombea udiwani wa Kata ya Ipagala, Gombo katika mkutano wa kampeni za CCM, Mtaa wa Mlimwa. 
Bura akipongezwa na Gombo baada ya kumuombea kura.
Mgombea Udiwani wa Kata ya Makole, Omary Haji akimpiga tafu mgombea mwenzie wa Kata ya Ipagala, Gombo.

Mgombea Udiwani wa Kata ya Ihumwa, Edward Magawa akimpigia kampeni mgombea mwenzie wa Kata ya Ipagala, Gombo.


Meza kuu wakinyoosha mikono ikiwa ni ishara ya kukubali kuwapigia kura wagombea wa CCM. Mgombea Urais wa CCM, Dk. John Magufuli, Mgombea Ubunge Dodoma Mjini, Anthony Mavunde na Diwani wa Kata hiyo ya Ipagala, Gombo.
Mgombea Udiwani wa Kata ya Ihumwa CCM, Edward Magawa akipongezwa na Mgombea Udiwani wa Kata ya Ipagala, Gombo baada ya kumfanyia kampeni katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Ipagala,Meshack Mkwanya akimnadi Gombo katika mkutano huo wa kampeni za CCM.
Gombo akishangilia pamoja na wana CCM baada ya mkutano huo wa kampeni kufana.

Gombo akiondoka baada ya mkutano kumalizika huku akilindwa.

Kwa Uhondo zaidi sikiliza clip hii ya Video hapo Chini.

 


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages